Saturday, February 5, 2011

Na hili ndilo Soko la kwanza apa Africa mashariki amabalo lilitumiwa na wakoloni na lina zaidi ya miaka 150 na mpaka leo lipo pale Bagamoyo na linaendelea kutumika daaah...

Wakati narudi Mjini kuna sehemu ya Tegeta nilikuta nguzo ya TANESCO imevunjika na nikaulizia ilivunjika lini nikaambiwa iyo nguzo ina miezi 2 sasa tangu ianguke! Sasa najiuliza kwanini hawa 'TANESCO' ni mahodari sana wa kupandisha Pesa ya umeme wao ilihali huduma zao ni mbovu na haziboreshwi? Mara mhao, mara bei ya umeme imepanda lakini huduma mbovu na hata kama m2 una pesa yako unataka kufungiwa 'LUKU' mpya basi utazungushwa weeeeee mpaka kucheee! yaani nahangaika kutafuta pesa yangu mwenyewe, jamani hata kuitumia pia nihangaike aaagh...

Ukisikia 'BODABODA' basi ndio hizi bwana, tatizo la ni kwamba kuanzia madereva wake mpaka abiria wanaowapakiza hawavai 'HELMET' ili kujikinga na ajali endapo itatokea, kuna watu wangu wa karibu kama 4 ivi wameshakufa kwa ajali ya Hizi hizi Bodaboda ila waliojeruhiwa naona itakuwa ni malaki kwa malaki maana Body ni mwili wako mwenyewe atiii...

No comments:

Website counter