Saturday, February 26, 2011

TUMSHAURI MWENZETU, 'HOUSEGAL' ATAKA KUPINDUA NDOA YA MTU JAMANIII...

Image

Kaka BEN KINYAIYA habari yako. Nategemea mzima wa afya na hutasita kunisaidia kunipa ushauri unaonifaa. Mimi ni mwanamke mwenye watoto wawili. Tangu nimeolewa miaka sita iliyopita, nimekuwa na msichana wangu wa kazi mmoja ambaye nimempenda sana hasa kwa kuwalea vizuri watoto wangu na kuwa mwepesi wa kazi. Kutokana na kuishi vizuri na ‘housigeli’ huyu, amekuwa kama mtoto wa nyumbani na hata ndugu zangu na wa mume wangu wanampenda sana na wamemzoea kupita kiasi.

Tatizo hili la kuwazoea ndugu wa mume wangu sasa naona linataka kuharibu ndoa yangu kwani huyu msichana ameanza tabia mbaya na amemweleza mkwe wangu kuwa mimi situlii nyumbani na sina muda wa kumshughulikia mume wangu kwani kazi zote anafanya yeye, mimi kazi yangu kusafiri na kushinda kazini. Huyu mama mkwe wangu kusikia hayo, amekuja juu na sasa anamshinikiza mume wangu aniache eti nashindwa kuhudumia nyumba na badala yake amuoe ‘housigeli’. Mume wangu ameshtuka na amenieleza kila kitu hali iliyonikasirisha sana.

Sasa naomba ushauri wako kwani mama mkwe bado yupo kwangu, je, nifanyeje kabla hajaondoka kurudi kwake? Mama Kelvin Tabata, Dar es Salaam.

3 comments:

Anonymous said...

kitu cha kwanza nashauri uchukue likizo hata kama bila malipo kama wiki mbili, ukianza likizo tu, mchukue huyo house girl bila kwamwalifu mtu yoyote wala mumeo usimwambie kitu, yaani usimpe muda wa kuaga mtu yoyote, ukifika ubungo bus stand umpe haki zake zoke hapo kituoni kisha mkabidhi konda au driver amshushe anakoelekea huyo msichana, pia umweleze huyo msichana kuwa hakuna sababu ya yeye kuendelea kuishi pale kwani umeamua kuacha kazi ili uhudumie nyumba yako na mumeo, baada ya hapo fanya mkakati wa kutafuta housegirl mwingine. Hapo utakuwa umesambaratisha mtandao, kwisha habari yaooo. Ni mimi mkereketwa "Pellagia"

Anonymous said...

Hiyo ndo picha ya mama anaetaka kuachwa? anaonekana kiwango. kama vipi amuache mumewe amuoe house girl halafu yeye ahamie kwangu.

Anonymous said...

Mi nafikiri uzuri ni mume yuko upande wa mkewe, kwa hiyo kabla ma mkwe hajaondoka aitishe kikao ma mkwe, mume , mke na house girl, halafu huyo mume amueleze ukweli. Mama yake assiingilie , na amueleze housegirl mbele ya kadamnasi haitatokea kuchukua nafas ya mkewe, na mke mtu ujitahidi kidogo kuhudumia mume

Website counter