Thursday, January 6, 2011

MTU WA NNE KWA UTAJIRI DUNIANI AONDOKA NCHINI...


Hatimaye huyu m2 hapo juu ambaye ni mtu wa 4 kwa utajiri Dunia Bw. MUKESH AMBANI ameondoka jana ndani ya Mbuga za wanyama za SERENGETI hapa kwetu Tanzania alipokuja kwa mapumziko ya X-mas na Mwaka mpya! Tajiri huyo anayeishi kwao nchini INDIA na anayelindwa kuliko OBAMA na aliyekuja na ndege 4 binafsi na kutua kwenye uwanja wa ndege wa Kilimanjaro anasema ameifurahia sana 'VAKESHENI' yake hapa Bongo na amesema kwamba kwanza amefikiria kujenga Hotel kubwa ya nyota 5 kama 'KEMPINSKY' ndani ya mbuga hizo na atatumia pia utashi wake kuwahimiza 'MATAJIRI' wenzie na taasisi na watu mbalimbali Duniani kuja kutembelea mbuga hizo na zinginezo zilizoko nchini na kujionea 'UBARIKIO' wa nchi yetu kwenye sekta ya Utalii, ila kilichomuhudhunisha tajiri huyu wa Dunia ni kitendo cha kushuhudia 'MZOGA' wa mmoja kati ya FARU 6 tulioletewa kutoka Africa Kusini aliyeuwawa na majangili ndani ya mbuga hizo! Tajiri huyo akiwemo waziri wa Maliasili na Utalii Mh. EZEKIEL MAIGE walikuta mzoga wa Faru huyo aitwae 'GEORGE' ukiwa umeshanyofolewa Pembe zake na Maharamia hao, kitendo kilichowahudhunisha wengi maana sasaivi ndani ya mbuga hizo wamebaki Faru watano tu kitendo kinachohatarisha wanyama hao Kutoweka kabsaa endapo hawatalindwa kwa ukaribu na askari wa Wanyamapori. Maoni yangu kwa Mh. waziri ni kuhakikisha hao 'maharamia' waliomuua huyo Faru wanakamatwa na kushtakiwa maana mie mwenyewe nawapenda sana Faru, sasa endapo wakitoweka itakuwaje? SITAKI kwenda Kenya eti nikawaone Faru looh, itakuwa aibu sanaaa duuh...

No comments:

Website counter