Thursday, January 6, 2011

KISOMO CHA MAREHEMU ABUU SEMHANDO WA TWANGA PEPETA KILIVYOKUWA...


Ivi ni vijimambo 2 siku ya 'KISOMO' cha mwanamuziki mkongwe wa Twanga Pepeta marehemu ABUU SEMHANDO kilichofanyika ndani ya ofisi za ASET pale Kinondoni jijini Dar ambapo mie nilikuwa ni Mwandazi mkuu kuhakikisha kilamtu alikula na kusaza kama unavyoona apo nahakikisha 'Shaba' ziko tayari kupakuliwa, na kazi hiyo niliifanya kwa ufasaha na hakuna aliyelalamika kwenye suala la msosi, maana kwenye kisomo watu badala ya kuja kufanya 'dua' ya kumwombea marehemu, basi wao wanakuja na 'ndizi' mfukoni ili kufakamia Biriani la msiba looh....

Hapo utafikiri Biriani nimeliweka 'Hamira' kudaadeki, maana si unaona mwenye Swahiba zangu walivyovimbilwa apo pembeni, we angalia 2 kitumbo cha RAY apo kilivyo 'Ndiii' na kulia apo ye KANUMBA anashushia na maji tartiiiiibuuuuu weeweee...

Mkurugenzi wa Twanga Pepeta ASHA BARAKA nae alikuwa ananiudhi sana maana kila mara alikuwa anachungulia jikoni akifikiri 'Biriani' haliji kwa kina mama, we angalia ilo jicho lake la 'Husda' apo loooh...

1 comment:

Anonymous said...

heee,jamani ni kweli watu huwa wanaenda na ndizi mfukoni?kama ni kweli basi watu hawafata kisomo,ila wamefata kula.mmh inasikitisha

Website counter