
Ivi ni vijimambo 2 siku ya 'KISOMO' cha mwanamuziki mkongwe wa Twanga Pepeta marehemu ABUU SEMHANDO kilichofanyika ndani ya ofisi za ASET pale Kinondoni jijini Dar ambapo mie nilikuwa ni Mwandazi mkuu kuhakikisha kilamtu alikula na kusaza kama unavyoona apo nahakikisha 'Shaba' ziko tayari kupakuliwa, na kazi hiyo niliifanya kwa ufasaha na hakuna aliyelalamika kwenye suala la msosi, maana kwenye kisomo watu badala ya kuja kufanya 'dua' ya kumwombea marehemu, basi wao wanakuja na 'ndizi' mfukoni ili kufakamia Biriani la msiba looh....
1 comment:
heee,jamani ni kweli watu huwa wanaenda na ndizi mfukoni?kama ni kweli basi watu hawafata kisomo,ila wamefata kula.mmh inasikitisha
Post a Comment