Saturday, January 8, 2011

JIACHIE NA BEN KINYAIYA....


Hiki kilikuwa ni kipindi chetu cha 'BEN & MAI live' cha wiki iliyopita ambapo tulikuwa na mshiriki wa Tanzania katika shindano la Tusker Project Farm na kushika nafasi ya pili aitwae PETER MSECHU na kwa hakika alitufurahisha sana wale woote waliohudhuria kipindi 'live' siku hiyo pale ndani ya studio za TBC mikocheni jijini Dar....

Yaaap Interview ilivyonoga nilikaa mpaka kwenye 'ZULIA' kuonesha msisitizo daah...

Tuache utani jamani mazoezi ni kitu muhimu, na mimi siku ukiniona nasakata kabumbu hutaamini, unaweza kusema kwenye UTANGAZAJI nilifata nini, na wala sikutanii ila kwa wanaojua kipaji changu kwenye soka hawashangai...

Kama kawaida yangu, nipo kama 'VAN NISTEROOY' ukidelay 2 nimekufunga kudaadeki, we chec ninavyoisubiria iyo Cross...

No comments:

Website counter