Saturday, January 8, 2011

HUYU NDIE MCHEZAJI PEKEE WA SOKA PICHA YAKE KUWEKWA KWENYE STAMP ZA BARUA, TUMSAIDIE APONE...

Waliojitokeza kumsaidi Mtagwa tunawapongeza Send to a friend

UONGOZI wa Chama cha Wachezaji wa Soka Tanzania (Sputanza) wanatarajia kumpeleka nahodha wa zamani wa Taifa Stars, Jellah Mtagwa mkoani Iringa kwa ajili ya kupatiwa matitabu ya ugonjwa wa Kiharusi unaomsumbua tangu mwaka 2006.

Hatua hiyo imechukuliwa siku chache baada kuandikwa habari kuhusu matatizo ya kiafya yanayomkabili kiungo huyo wa zamani wa Stars kiasi cha kumsababishia kushindwa kumudu gharama za matibabu ikiwa ni pamoja na kujikimu kimaisha na familia yake.

Baada ya kuandikwa habari za Mtagwa, alitokea msamaria mmoja ambaye amejitolea kumchukua mchezaji huyo wa zamani kwa ajili ya kwenda kupata matibabu mkoani humo, pia wapo waliojitokeza kumsaidia kwa kutoa fedha.

Kitendo cha wadau mbalimbali kujitokeza kumsaidia mchezaji huyu ni kitendo cha kizalendo na kinapaswa kuungwa mkono na wanamichezo wote nchini kutokana na mfumo wa michezo ulivyo nchini unaosababisha wachezaji wengi kuishi maisha magumu wakishastaafu katika michezo mbalimbali.

Tunaamini utamaduni wa kuchangia matibabu kwa wanamichezo wetu ndio tija kwa maendeleo ya taifa na michezo kuliko ule wa kusubili msiba ndipo tunajitokeza kugharamia gharama za mazishi.

Sasa wakati umefika kwa Sputanza kwa kushirikiana na TFF, klabu kuandaa utaratibu wa kukusanya fedha kwa ajili ya kuwasaidia wachezaji wakongwe nchini na kuhakikisha unakuwepo mfumo wa kuwasaidia wachezaji wanapostaafu.

Vyama hivi kwa kushirikiana na klabu kwa kuanzia vinaweza kuandaa mechi za kirafiki hapa jijini Dar es Salaam na mikoani na fedha za viingilio zikatumika kwa ajili ya kugharamia matibabu ya wachezaji.

No comments:

Website counter