Tuesday, January 4, 2011


Hapa nikiwa na mdau USHER RAYMOND tukifuatilia Onyesho la mapacha usiku huu wa leo Jumanne ndani ya ukumbi wa Coco Beach, ilikuwa balaa...

Hawa ni wanenguaji wakongwe ila wenye kiwango kikubwa sana, kushoto ni MARIAM 'ZIDANE' ambaye kwa wale wapenzi wa Diamond sound 'Wana Nkibinda Nkoe' enzi zile watakuwa wanamkumbuka sana kwa uhodari wake, na kulia ni MARIAM 'BERCY' ambaye kwangu mimi hapa mjini kwenye hizi Bendi hakuna Mnenguaji mwenye 'NYONGA' lainiiii kama huyu na kama unabisha basi jaribu kwenda 'MAPACHA' sikumoja kushuhudia ukweli ninaokwambia, yaani utadhani hana 'mfupa' bwana daah...

STEVE NYERERE nae alikuwepo kuuza 'NYAGO' kama kawa looh...

Ilikuwa ni SEBENE kwa kwenda mbele alaah...

No comments:

Website counter