Friday, December 17, 2010

KWAHERI YA KUONANA RAMADHANI MTORO ONGALLA...


Mwili wa aliyekuwa mkongwe wa muziki nchini na barani Africa marehemu REMMY ONGALLA ukiwa ndani ya Jeneza wakati wapenzi na mashabiki wake wakimuaga kwa mara ya mwisho kabla ya kupelekwa kwenye nyumba yake ya milele. Ntamkumbuka sana kwa tungo zake za maana na zenye kuona mbali na haswa pale alipowahi kuimba wimbo wake uitwao 'MAMBO MAMBO KWA SOKSI', miaka iyo na mpaka wimbo huo ukapigwa marufuku kupigwa Redioni wakati huo lakini leo hii mpaka mapadri wanahimiza matumizi ya Condom! Hapo ndipo utaamini kweli Remmy alikuwa anaona mbali, pumzika kwa amani Baba...

Nilihakikisha na mimi ninakwenda kumuaga Dk REMMY ONGALLA, mtu aliyetunga wimbo mzuri sana ninaoupenda uitwao 'SAUTI YA MNYONGE'

Katikati ni mtoto wa kiume wa Dk Remmy ambaye ni rafiki yangu mkubwa aitwae KALLY anayechezea timu ya AZAM FC ya jijini Dar akiwa na majonzi makubwa baada ya kumuaga Babake jana...

Kulikuwa na watu wengi waliokuja kumuaga Dk REMMY na hapa nikiwa na Mkongwe wa muziki kutoka Congo BOZI BOZIANA ambaye ameondoka jana kurudi Paris anakoishi sasa, pamoja na ASHA BARAKA na STEVE NYERERE...

Na hapa kihojiwa na vyombo vya habari mbalimbali kuhusiana na msiba huo mkubwa...

No comments:

Website counter