Sunday, December 19, 2010

INABIDI HAWA VIONGOZI WENGINE WA AINA HII WACHAPWE VIBOKO WALLAH...


Juzi nilipita hii barabara ya Victoria kuelekea Mwenge apa jijini Dar nikakuta kuna MBWA tena mbichi aligongwa barabara usiku wake na mchana huo kilaq gari lilikuwa linakwepa kuukanyaga mwili wa mbwa huyo maana ulikuwa bado Mbichi kabsaaa! Sasa cha kushangaza leo mchana huu nimepita tena kwenye barabara hiyo na sehemu ileile nikakuta Ule mwili wa yule Mbwa bado upo ila kwasasa umeshakanyagwa sanaa na magari na kupondeka na hatimaye kukauka, sasa najiuliza tangu majuzi Halmashauri ya Wilaya ya Kinondoni na haswa wale wanaofagia barabara kilasiku hawakuuona 'Mzoga' huo tangu juzi? maana sasaivi imekuja ni jambo la kawaida kwa barabara za apa Dar kukuta mizoga katikati ya barabara, kwanini sehemu husika hazibadiliki kiutendaji? Au mpaka msikie Rais anapita ndio mkurupuke kusafisha na kukarabati barabara eeeh...

No comments:

Website counter