


Huyu mzee anaitwa WARREN BUFFETT,ni mtu watatu kwa utajiri Dunia hii na ni mzaliwa wa Marekani mwenye umri wa miaka 79. Ni mmiliki wa kampuni ya BERKSHIRE HATHAWAY mwenye utajiri wa Dolla Billinoni 47 mwenye makazi yake mjini Omaha Nebraska na ni Mhitimu wa shahada ya Uzamili ya Sayansi kutoka Chuo kikuu cha COLUMBIA. Huyu nae ameshafiwa na mke wake ila ana watoto 3.

Huyu ni muhindi aitwae MUKESH AMBANI mweny umri wa miaka 53 mkazi wa Mumbai kule INDIA. Yeye ni mtu wa nne kwa utajiri Duniani na amerithi na kuiendeleza Kampuni ya Familia yake inayojihusisha na Ujenzi na Mafuta. Jamaa ana utajiri wa Dolla Billioni 29 ingawa hakumaliza Shahada yake ya Uzamili katika chuo kikuu cha Bombay kule India na ameona na kupata watoto 3! Sasa fikiria tajiri kama huyu ana watoto watatu amemaliza, sasa weye 'mbongo' mwenzangu kapuku watoto '9' wa kazi gani jamani wakati una njaa inakukabili...

Huyu bwana ni mtu wa tano kwa utajiri Sayari hii na anaitwa LAKSHMI MITTAL, ana umri wa 59 na ni mzaliwa wa INDIA ila makazi yake kwasasa ni jijini LONDON Uwingereza. amerithi Kampuni ya Gesi na Mafuta kutoka kwa Babake, ana umri wa miaka 59 na ni mhitimu wa shahada ya Sayansi na Sanaa kutoka chuo kikuu cha CALCUTTA. Ana utajiri wa Dolla Billioni 28.7 ila fikiria jamaa ana watoto 2 tu, msichana na mvulana Daaah...
2 comments:
asante kwakutujuza wengine ambao tulikuwa hatujuii endelea kijana kutuletea habari motomoto ubarikiwe
abromovich wangapi
Post a Comment