Wednesday, December 8, 2010

BREAKING NEWZZZZ, CHOKORAAA, KALALA JUNIOR NA JOSE MARA OUT FM ACADEMIA NA TWANGA PEPETA KUANZIA JANA...


Huyu ndie JOSE MARA, mwimbaji mwenye sauti tamu na kipenzi cha mashabiki wengi wa bendi yake ya FM ACADEMIA aka 'Wazee wa ngwasuma', ni mmoja kati ya vijana watatu wanaounda kundi zima linalotamba apa mjini liitwalo 'MAPACHA WATATU' akiwa na wenzie kina Khalid Chuma 'Chokoraa' na Kalala Junior wa Twanga Pepeta! Sasa hawa vijana watatu ambao mwanzo walimshawishi na mwenzao Chalz Baba kutoka Twanga pepeta lakini 'akachomoa' kujiunga nao na akabaki kutulia na Twanga! Sasa jana huyu Jose Mara inasemekana amepewa Barua ya kusimamishwa kazi na Bendi baada ya kukaidi onyo la kutoenda kuimba kwenye iyo Bendi yao ya 'Mapacha Watatu' jana usiku kwenye ukumbi wa Fukwe za Coco Beach apa jijini Dar, kwaiyo inasemekana kashafukuzwa FM ACADEMIA daaah...

Hii picha ni ya jana usiku mnene nikiwa na aliyekuwa Rapa na mwimbaji wa Twanga Pepeta KHALID CHUMA 'chokoraa' nilipoenda pale Coco Beach kushuhudia kama kweli huyu bwana atapanda kuimba na kundi lake la 'Mapacha Watatu' au ataenda kuimba na Bendi yake ya TWANGA PEPETA pale Top Life Kinondoni? Sasa matokeo yake jamaa ameikacha Twanga pepeta na kwenda kuimba kwenye kundi lao na kwa maana hiyo kwa mujibu wa barua aliopewa jana mchana na Bendi yake ya Twanga Pepeta kwamba asipofika kazini usiku basi atakuwa amejifukuzisha mwenyewe kazi, kwaiyo jamaa ndio ivyo tena Rapa wenu mumpendae ameshafukuzwa kazi TWANGA PEPETA kuanzia jana usiku daah...

Huyu ndie CHALZ BABA mwimbaji hodari wa bendi ya Twanga Pepeta ambaye inasemekana ndie kavuruga 'mpango mzima' baada ya kuchomoa kujiunga na Kundi la 'MAPACHA WANNE' ila baada ya yeye kujitoa jina likabadilika wakajiita 'MAPACHA WATATU' ivyo wakabaki Jose Mara, Chokoraa na Kalala junior! Na hapa ilikuwa ni jana usiku ndani ya ukumbi wa Top Life Kinondoni wakati Twanga Pepeta ikitumbuiza na wakati huo huo wenzake wakiwa wanatumbuiza pale Coco Beach...

Nikiwa Top Life Kinondoni nimepozi na wanamuziki wa Twanga Pepeta, kushoto ni VICTOR MKAMBI na kulia ni Rapa MSAFIRI DIOF, na kwa 'umbea' wangu nilienda kushuhudia kama kweli kina Kalala Junior na Chokoraa watakuja kuimba apo kazini kwao 'Twanga' au wataikacha na kwenda kuimba kwenye kundi lao la 'Mapacha Watatu' kule COCO na kukuta Holaaaaa hawapo babu kwaiyo na kibarua kimeota majani duuuh...

Wanenguaji wa Twanga wakifanya kufuru jana usiku pale Top Life Kinondoni...

2 comments:

Anonymous said...

umejishtukia mmbea eeh...mi naona poa tu mapacha watatu watatoka wakaze buti

Anonymous said...

Kinyaiya sasa umeboa maana unaandika mambo ya kizushi kaka. Mbona nimemuona jose kwenye jukwaa la FM pale mlimani city kwenye sherehe ya air tel.
Jaribu kuwa makini nablog yako kaka vinginevyo uza sura na bia.

Website counter