Wednesday, November 10, 2010

PICHA HII IMENIPELEKA MBALI NA 'KUNIHUDHUNISHA' SAANAAA KIMAWAZO....


Nimeiangalia kwa makini picha hii na kwa hakika imenitoa machozi maana imenifanya niwaze mbali saana na kutamani nimuone kwa macho yangu huyo mtoto hapo kama bado yuko hai kwasasa! Ebu jaribu kuwa na moyo wa kibinaadamu wa kuweza kuwafikiria wenye shida maana Mungu ana sababu yake kuwaweka watu kwa matabaka tofauti, wengine kawaumba wawe matajiri na wengine wwawe masikini ili nyie matajiri muweze kuwasaidia wenzenu, na usijione apo ulipo unakula mara 3 kwa siku, kuna wengine hata mara moja tu ni shida na ukitaka kuamini jaribu kufikiria uyo apo juu kwenye picha alivyokonda na kujiinamia kwa maumivu makali, je unadhani anawaza nini moyoni na kichwani mwake?Plz tuwafariji wenye shida na ndio maana nikamkumbuka mwanamuziki maarufu wa BURUNDI KHADIJA NIN ambae nilikutana nae mjini BRUSSELS BELGIUM anakoishi mwaka jana nilipokuwa uko akanipa hii CD ya Album yake na kati ya nyimbo zoote huo apo juu ndio niliupenda zaidi kwakua unatoa ujumbe mkubwa kwa watu kuwasaidia masikini wanatuzunguka popote pale tulipo...

3 comments:

Masangu Matondo Nzuzullima said...

Picha hii ni mojawapo ya picha za muhimu sana katika karne iliyopita na ilisaidia katika kuuamsha ulimwengu wa Kimagharibi kuhusu janga la njaa lililokuwa likiikumba Ethiopia katika miaka ya 70 na 80. Ilitonesha milizamu nyingi na misaada ikaanza kumiminika. Hata hivyo sijui kama tumejifunza lolote kwani mambo bado ni yale yale - hakuna mikakati ya maana ili kuhakikisha kwamba hali kama hii haijirudii tena.

Kupitia katika picha hii pia waweza kuuona msimbo tata wa kimaumbile. Mtoto anakaribia kukata roho kwa kukosa chakula na wakati huo huo tai naye anasubiri ajipatie chakula. Ndiyo maisha ati!

Anonymous said...

mpiga picha hii alichaguliwa kama amepiga picha bora ya mwaka lakini aliwahi kuhojiwa kwa nn akumsaidia huyo mtoto maana baada ya kupiga picha alimwacha na kwenda zake na inasemekana mtoto huyu alikufa. Baadae mpiga picha alijiua kwa msongo wa mawazo baada ya ulimwengu kumshambulia kuwa alifanya ukatili kumwacha binadamu mwenzio katika hali kama ile wakati alikuwa na uwezo wa kumwokoa

Anonymous said...

MM mwenye nilisha iyona mara nyingi sn nakila nikiitazama ninalia moyo unauma sana na ninashidwa kupata nguvu......

Website counter