Tuesday, November 16, 2010

NAWALAANI ENYI VIBAKA MLIOMVAMIA NA KUMUUMIZA '20 PERCENT' LOOOH....


Sikuzote namzimia huyu mshkaji kwa nyimbo zake makini zenye ujumbe mkali ndani yake ambayo unapoimba popote kama uligombana na mtu anaweza kudhani labda 'unamfumbia' mafumbo kume waalaaa! Kijana ana kipaji kikubwa ila kinachoniacha hoi kwake ni kitendo cha kutoonekana ovyo 'Mjini' maana hafanyi Concert popote na wala sijawahi kumuona akifanyiwa 'Interview' na TV yoyote apa nchini, yaani yupo kama 'Digidigi' aaah! Ila juzijuzi alikuwa Mjini Bukoba kwa ajili ya kurekodi FILAMU yake inayoelezea maisha yake halisi but alivamiwa na Vibaka usiku na kumjeruhi vibaya kichwani kiasi cha kunyolewa nywele zoote na hivyo kumfanya asitishe zoezi la kurekodi mwendelezo wa Filamu hiyo maana alitakiwa kuwa na nywele ndefu zilezile alizoanza kurekodi nazo Filamu iyo tangu mwanzo! Pole sana swahiba kwenye moja ya nyimbo zako ulizoimba ukisema 'Vibaka wakikuibia wanakurudisha nyuma', na ndivyo ilivyokutokea kwako mwenyeeeweee baba! Uchec huo wimbo wake wa 'Malumbano' apo chini, yaani ninaupenda kishenzi....

3 comments:

Anonymous said...

Beny thanks kwa taarifa ya huyu kaka nampa pole sana na kuwalaani vibaka hao, ila Beny 20% amewahi kuhojiwa na sauda mwilima mara moja tu, ukweli ni kwamba jamaa sio bishoo hata ungebahatika kuangalia kipindi cha sauda yaani ni mtu makini anaongea kiswahili chake fasaha sio wengine wakig'aa kidogo wats zinakuwa nyiiiiiiiingi sasa Beny si umualike kwenye kile kipindi chetu na maimartha? ukweli kijana yuko juu sana basi tu ni vile sio bishoo! big up 20% tuwekee na wimbo wake TAMAA MBAYA basi Beny. Mama Richie Moshii

Anonymous said...

Kuna wimbo wake wa tamaa mbaya ameongelea kuhusu wezi kama ufuatavyo

" Najaribu kukuasa wewe kijana jaribu kuacha mambo ya kuibiana na kama haiwezekani siku tukionana nitakiweka mbali kisimu changu cha mchinaaaa, mwenzenu naona noma polisi kupelekanaaaaa"

Anonymous said...

Watanzania hawataki mtanzania mwenzao aendelee mbele kama hawa vibaka kawakosa nn huyu jamaa wakati yeye ni msanii tu, sijui useme nn kuhusu hawa vibaka ni watu si wa kuishi katika nchi yetu hii yenye amani na utulivu kama kuna uwezekano kuwajua ni kuwamaliza kabisa, hawana ubinadamu hata kidogo lakini atakulipia wataku fa kama mbwa barabarani.

Website counter