Friday, November 19, 2010

HAWA NDIO WANASOKA WA KUIGWA BARANI AFRICA...


Huyu kiungo 'General' wa pale darajani CHELSEA FC, MICHAEL ESSIEN, mzaliwa wa eneo la Awutu Breku mwendo wa masaa mawili kutoka mjini Accra. Huyu ni mmoja kati ya wanasoka wachache wa Kiafrica wanaokumbuka nyumbani baada ya kuzichuma kwa wingi uko na katika picha hii iliyopigwa Jumanne hii wakati anawasili mjini Accra kwa ajili ya uzinduzi wa Mfuko wake wa kusaidia jamii na vijana wenye vipaji tofauti kwa kujenga Hostel itakayowakusanya vijana wenye vipaji mbalimbali na kisha kuviendeleza ikiwemo kuwatafutia timu barani Ulaya, na ukimuuliza sababu ya kufungua kituo icho atakujibu ni vile yeye alivyosulubika kupata mafanikio aliyonayo sasa, na ivi sasa amenunua mtaa mzima sehemu moja mjini Accra na kuwaweka ndugu zake mbalimbali daah...

Anaitwa SAMUEL ETO'O FILLS, mzaliwa wa kule DOUALA nchini CAMEROON ambaye kwangu mimi ndie mshambuliaji hatari zaidi Duniani akiwa kwenye eneo la 'mita 18' ndani ya BOX! Yeye ameamua kwenda kijijini kwao walikozaliwa wazazi wake na kutengeneza barabara za viunga vyoote vya kijiji icho na kuweka visima vya maji kuzunguka kijiji kizima pamoja na kujenga Zahanati pamoja na kutoa misaada kwa timu mbalimbali za soka nchini humo! Huwa na ratiba ya kwenda kutembela kijiji icho wakati wa sikukuu na kwa jinsi anavyopendwa, wanakijiji wakishapata taarifa za ujio wake basi kila mtu anakwenda kununu kitenge na kutandika chini kwenye barabara wakati msafara wa mchezaji huyo ukipita, yoote hiyo ni kumuonesha heshima kwa moyo wake wa kujitolea kwao, na kwasasa anachezea Inter Milan ya ITALIA......

Huyu anaitwa NWANKO CHRISTIAN KANU, mzaliwa wa Owerri kule nchini NIGERIA! Yeye atakumbukwa kwa kuanzisha Hospital ya kutibu magonjwa ya 'moyo' baada ya yeye mwenyewe kunusurika kufa kwa uggonjwa huo wakati huo anaichezea timu ya Inter Milan ya ITALIA! Anaamini kwamba 'ugonjwa huo' ulimkuta yeye akiwa tayari ni mtu anayejiweza, je ni wangapi wamekufa kwa ugonjwa huo kwa kukosa pesa ya matibabu ya uhakika? Kwasasa anamalizia mkataba wake na klabu ya PORTSMOUTH ya England.

No comments:

Website counter