Monday, November 8, 2010

JAMANI SERIKALI EBU FANYENI MPANGO WA MATIBABU YA 'MTUMISHI' WENU HUYU MKONGWE...

DC wa zamani hoi kitandani Send to a friend


Aliyewahi kuwa Mkuu wa Wilaya ya Mbalali, Mkoani Iringa Hawa Ngurume, akizungumza na waandishi wa habari wa gazeti hili, nyumbani kwake Goba Kinzidi, Dar es Salaama jana, kuhusu maradhi ya figo yanayomsumbua. Picha na Venance Nestory


ALIYEKUWA mkuu wa Wilaya ya Mbarali, Hawa Ngulume yuko katika hali mbaya nyumbani kwake, Goba Kinzudi jijini Dar es Salaam akisumbuliwa na ugonjwa wa vichomi na mapafu.

"Nimeona nitumie chombo cha habari kufikisha ujumbe (wa ugonjwa) kabla sijafa,” alisema mkuu huyo wa zamani.

Akizungumza nyumbani kwake jana, Ngulume alisema kwa miezi mitatu sasa yuko hoi na hawezi kutembea bila kusaidiwa na hivyo anaiomba serikali imsaidie aweze kwenda kutibiwa nje ya nchi.
Alisema ameamua kutumia gazeti hili kufikisha ujumbe kwa serikali na CCM kuhusu maradhi yanayomsumbua baada ya njia nyingine kushindikana.

“Nilipeleka taarifa kwnye chama changu kwamba ninaumwa nahitaji msaada, lakini sikujibiwa; pia nimefanya juhudi za kutaka kumwona Waziri Mkuu ili anisaidie, lakini juhudi hazikuzaa matunda. Nimeona nitumie chombo cha habari kufikisha ujumbe kabla sijafa,” alisema.

Ngulume, ambaye ni kada maarufu wa CCM aliyetumikia nafasi ya ukuu wa wilaya kwa miaka 18, alisema maradhi hayo yalianza kumsumbua baada ya kumalizika kwa mchakato wa kura za maoni za chama hicho.

Alisema aliomba ridhaa ya chama hicho kimsimamishe kuwa mgombea ubunge katika Jimbo la Singida Mjini.
“Katika mchakato ule Mohammed Dewji alishinda, na mimi nikawa mshindi wa pili. Niliporudi Dar es Salaam nikaanza kujiandaa kwenda kumpigia debe mshindi kama ulivyo utaratibu wa chama chetu, ndipo nikaanza kuumwa ghafla,” alisema.

Mkuu huyo wa zamani wa wilaya ambaye amewahi kushika wadhifa huo kwenye wilaya mbalimbali zikiwemo za Bagamoyo, Ilala na Kibaha, alisema amekuwa akitibiwa katika hospitali za Lugalo, IMTU na Ocean Road
“Kuna kipimo ambacho nilitakiwa kuwekewa kwenye kinywa katika Hospitali ya Ocean Road ili kiweze kubaini kama kwenye mapafu kuna maji au la, lakini ilishindikana kwa sababu ya kukosa pumzi, na hawana kipimo cha aina nyingine,” alisema.

Alishauriwa kwamba aendde India ambako kuna vipimo vya aina nyingi ambavyo havihitaji kuwekwa katika kinywa na kwamba vipimo hivyo vingemfaa kutokana na matatizo yake ya pumzi.

Alisema katika kuhangaika alifika katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, lakini cha kushangaza alikaa kuanzia saa 8.00 mchana hadi saa 11.00 jioni bila kuhudumiwa.

“Ndipo mtu mmoja anayenifahamu aliyekuwa akipita nilipoketi, akanisalimia kwa kuniita mheshimiwa. Muuguzi mmoja jina ninalihifadhi akaja kutaka kunihudumia, nikamwambia ina maana siwezi kupata huduma hadi niwe mheshimiwa, nikaondoka kwa hasira," alisema.

Alisema baada ya kutelekezwa na kunyanyapaliwa Muhimbili, amekuwa akipata matibabu kwenye hospitali za binafsi kwa ajili ya kutuliza maumivu.

“Maumivu ninayoyapata ni makali sana, nina vichomi utadhani kuna msumemo unaokata viungo vyangu ndani ya tumbo. Ninalia usiku kuchwa kwa maumivu, wanaonisaidia ni majirani tu ambao hufika kila mara kunijulia hali,” alisema.

No comments:

Website counter