Friday, November 12, 2010

HEEE HII 'KAULI' IMEKAAJE TENAAA....

Tegete amshangaa kocha Taifa Stars Send to a friend


Kocha wa timu ya Taifa stars,Jan Poulsen


SIKU moja baada ya kocha wa timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars na Kilimanjaro Stars, Jan Poulsen kutangaza kikosi chake kwa ajili ya michuano ya Chalenji, mshambuliaji wa Yanga aliyeachwa, Jerry Tegete amemshangaa kumwita Gaudence Mwaikimba na kumwacha.

Juzi, Jan Poulsen alitangaza kikosi chake kujiandaa na mechi za kimataifa za FIFA Novemba 17 na Kombe la Chalenji, michuano itakayoanza Novemba 27 hadi Desemba 11.

"Aah! unajua nimeshangaa, yaani kocha ananiacha mimi anamchukua Mwaikimba (Gaudence)? lakini ni uamuzi wa mwalimu...mimi naamini natisha ndiyo maana naongoza kwa mabao," alisema Tegete jana.

Alisema kuwa anashangazwa na kocha huyo kumuacha katika kikosi chake pamoja na juhudi yote anayoonyesha katika timu yake.

Hata hivyo, alisema kocha ndiye mwenye kuangalia wachezaji na huenda ameona kuwa kiwango chake (Tegete) hakifai kuichezea timu yake.

Mwaikimba, mshambuliaji wa Kagera Sugar alielezea kufurahishwa na kuitwa kwake tena na Poulsen.

Mshambuliaji huyo aliyetokea Ashanti FC ya Ilala kabla ya kujiunga Yanga, alikuwa miongoni mwa wachezaji wa mwanzoni katika kikosi cha aliyekuwa kocha wa timu hiyo, Marcio Maximo.

Hata hivyo, 'alichakachuliwa' katika kikosi cha Stars kutokana na kushuka kiwango kabla ya kuitwa tena juzi.

Mwaikimba alisema mpira unachezwa ndani na nje ya uwanja na endapo watu hawatampa ushirikiano watafanya wachezaji wajione wanyonge na kufanya vibaya katika michezo yao.

Naye mshambuliaji wa Simba, Mussa Hassan Mgosi amesema kuwa kuachwa kwake katika kikosi cha Jan Poulsen ni kutokana na kuporomoka kwa kiwango chake.

Alisema kuwa amecheza chini ya kiwango kutokana na maumivu ya mguu yaliokuwa yanayomsumbua lakini ana imani kuwa atajitaidi kurudisha kiwango chake katika raundi ya pili ya Ligi Kuu Tanzania Bara mwakani.

Timu hiyo ya Kilimanjaro Stars inaanza maandalizi yake ya kujiandaa na michuano ya Chalenji ambapo watafungua dimba na Zambia siku hiyo.

No comments:

Website counter