Saturday, November 6, 2010

HAYAAA DK, NI AWAMU YAKO NYINGINE TENA ILA SIKIA HII....


Hayaa DK KIKWETE leo tumekukabidhi nchi wewe na huyo makamu wako Dk BILAL, sasa wananchi wanataka kuona malalamiko yanapungua kwa kuyafanyia kazi mapungufu yyote yaliyojitokeza tangu ushike Hatamu! Bado kuna malalmiko ya watu kunywa maji machafu ambayo hata Punda hafai kuyanywa! UFISADI upungue maana najua kuutokomeza itakuwa ngumu na uwaadabishe wale woote wenye tuhuma za waziwazi ambazo kila m2 NJI hii anajua na kuwajua vilevile! Kule machimboni madini ye2 myanazidi kuzolewa bila wananchi kufaidika ipasavyo na matokeo yake tunaachiwa 'MAHANDAKI' makubwa makubwa daah! Kuna hili la 'watu wako' kusaini mikataba 'feki' ambayo inatuingizia Hasara kilasiku ambayo matokeo yake wakikamatwa wanafungwa miaka 2 kisha wanaingia tena kitaa kama kawa na wala hizo pesa 'walizokwiba' hawanyang'anywi! Alafu mwisho nakupa siri moja Mh, ukitaka ufanikiwe kwenye Awamu yako ya sasa, chukua 'mashtaka' yooote ambayo kina SLAA na wenzake walikuwa wanayapigia debe kwenye kampeni zao uyafanyie kazi na kuyatatua maana mengine ni ya ukweli kabsaaa kaka...

2 comments:

Anonymous said...

We kinyaiya kumbe na wewe ni msanii wakuchakachua. Unbelievable kweli nchi imekwisha!. Unategemea kweli JK adi-sturb self interest zake. Wapi bana!

Anonymous said...

sio siri nimegundua something in you kaka,sitasema mengi lkn I LOVE U.(Sio kimapenzi,kindugu tu).
TUKO PAMOJA MUNGU ATATUSAIDIA WANYONGE WAKE.

Website counter