Friday, October 29, 2010

MJUE MFUNGWA ALIYEPATA SHAHADA YA SHERIA AKIWA GEREZANI UKONGA...


Nilikuwa sijui ila kumbe ukiwa na nia popote pale unaweza kufanikiwa jambo lako kama jamaa huyu alivyotimiza ndoto yake tena akiwa GEREZANI daah! Anaitwa MICHAEL SEMAYOGA, mfungwa aliyehukumiwa kifungo cha miaka 10 tangu mwaka 2002 uko Gerezani nchini Ushelisheli kabla ya kuhamishiwa kutumikia kifungo chake kwa tuhuma za kujihusisha na madawa ya kulevya! Kutokana na kujua Lugha ya Kiingereza kuliko wafungwa wengine kulikomfanya awe kama mkalimani wao kwa mambo yoote ya sheria na Lugha gerezani humo, alipata msukumo wa kusoma akiwa Gerezani humo baada ya kumuona mfungwa mwingine aitwae HARUNA PEMBE ambaye alikuwa anasomea Sheria katika Chuo kikuu Huria Tanzania 'OUT' akiwa ndani Gerezani. Anakumbuka shida ya kusoma katika mwanga hafifu Gerezani humu hali iliyomfanya kuvaa miwani kwasasa, na anasema alikuwa akitii sheria za Gerezani kama vile kufanya kazi ngumu na kulala mapema saa 2 kamili usiku ma 'shurba' zingine ila kwasasa anashukuru mungu na kujiona 'mtu' mpya kutokana na Elimu aliyopata! HONGERA SANA kaka Michael kwa ujasiri wako na muda si mrefu utafaidi matunda ya uvumilivu wako, SALUT...

No comments:

Website counter