Saturday, October 30, 2010

DAIMA NITAKUKUMBUKA 'MWANANGU' MZIRAY...


Pumzika kwa Amani kaka SYLESAID MZIRAY, pumzika salama rafiki, pumzika salama mtani na kwa hakika nitakukumbuka saanaaa! Kwako wewe hawakukosea kukuita SUPER COACH kutokana na ujuzi wako uliobobea kwenye ufundishaji soka apa nchini tangu enzi za PLISNER, PAN AFRICA, YANGA, SIMBA na Timu ya Taifa 'TAIFA STARZ'. Kwangu mimi Binafsi namkumbuka kwa mambo mengi kila tulipoonana! Ni mtu mwenye kupenda utani sana na haswa anapopenda kulitumia neno 'mwanangu' kila mara! Namkumbuka kwa jinsi alivyokuwa shabiki wangu mkubwa wa vipindi vyangu vya kwenye TV ambapo alinishangaza kwa kunikumbusha kila nilichofanya au watu niliowahoji kwenye vipindi vyangu mbalimbali vilivyopita na mwisho kabisa nakumbuka kwa mara ya mwisho kukutana katika uwanja wa TANGANYIKA PACKERS ambako timu ya SIMBA aliyokuwa anaifundisha ilikuwa ikifanya mazoezi wakati huo alivyoninunulia 'Ice Cream' ya Azam za kwenye Baiskeli tena bila kujua baada ya kumuita muuzaji akachukua yeye kwanza kisha akamwambia muuzaji aniulize kama nilipenda kula Ice cream, nami nilikubali kwa heshma yake nae akanilipia 'Buku' la Ice cream hiyo, ASANTE MZIRAY NA NITAKUKUMBUKA SANA 'MWANANGU', mungu akulaze mahali pema rafiki yangu, AMEIN...

No comments:

Website counter