Sunday, June 20, 2010

WATU WALIVYOKULA BATA JANA USIKU PALE MZALENDO KIJITONYAMA JIJINI DAR....


Nikiwa na mzee wa Commercial AMBWENE YESSAYA aka 'AY' ndani ya kiwanja cha MZALENDO kilichopo Kijitonyama. Nilichopenda kutoka kwa huyu bwana ni kitendo chake cha kutumia jina lake asilia la 'Kinyumbani' tofauti na watu wengine walio na majina ya Kithungu ilihali ni mkabila wa kitanzania, maana utakuta m2 anaitwa ROBERT MAC FADDEN MARTIN, ukimuuliza we kabila gani atakwambia MNGONI wa TUNDURU! na ukimwambia mbona mie nilitegemea utalitumia jina lako la Ukoo kama vile MBAWALLA, KOMBA na mengineyo basi mtakosana na pengine ugomvi kutokea! Nakupa mfano mdogo sana, kule nchini Congo kumewekwa Sheria kwamba lazma mtu utumie jina lako la ukoo, sheria hiyo iliwekwa na aliyekuwa Rais wao ambaye jina lake aliitwa MOBUTU SESESEKO KUKU NGEHBU WA ZABANGA! sasa chec ilo jina lake lilivyo, na hata nchi wakati wa utawala wake aliita ZAIRE ila baada ya kufa 2 mijitu mingine ikabadili jina la nchi na kuiita CONGO! Sasa wadau mie nauliza hii tabia ya kutumia zaidi majina ya kizungu ilihali ni mzawa imekaaje jamanii...

DJ BIKE wa RADIO ONE akiserebuka na mipini ya Oldies ndani ya viwanja vya mzalendo jana usiku...

No comments:

Website counter