Tuesday, October 5, 2010

NILIPOTEMBELEA MAZOEZI YA TWANGA PEPETA JANA MCHANA...


Hapa mazoezi yaliponikolea nikaamua kupiga Tumba baada ya kuziona ziko wazi alaaaah...


Amini usiamini, huyu aliyeko kushoto ndie VICTOR MKAMBI aka 'Proffesionale keyboadist' na huyo aliyeko kulia kwenye Dram ni kijana mdogo sana kiumri ila ndie 'ROHO' ya bendi nzima ya TWANGA PEPETA aitwae JAMES KIBOSHO! amini maneno yangu, huyo kijana ndie alibadilisha MELODY nzima ya bendi Twanga Pepeta kwa upigaji 'Dram' wake wa kisasa kabisaa na ukitaka ugombane na watu wa Twanga basi wasikie unamzengea kijana uyo eti utake 'kumuhamisha' bendi nyingine, nakwambia watakutoa 'Mshipa' wallaah...

Huyo mwenye Gitar ndie KALALA JUNIOR, mwimbaji mahiri wa Bendi hiyo ya Twanga Pepeta ila ana sifa moja kubwa inayomfanya wamuabudu kwenye Bendi hiyo, nayo ni kwamba ndie 'Mwanamuziki pekee katika Bendi hiyo anayepiga vyombo vyoooote'....

Squad nzima ya Madansa wa Bendi iyo wakipiga Tizi la nguvu wakiongozwa na AISHA MADINDA, aliyeko katikati mwenye Jezi, ila naskia amerudia ule mchezo wake wa kuvuta 'naniiliuuu'....

No comments:

Website counter