Sunday, July 4, 2010

WAZAZI WA ASAMOAH WAFANYIWA FUJO GHANA...


Ingawa Waghana na waafrica kwa ujumla wamefurahi hatua iliyofikiwa na Timu ya taifa ya GHANA kuingia robo fainali kwenye michuano ya kombe la dunia inayoendelea uko nchini Africa ya Kusini, lakini baadhi ya mashabiki wa soka nchini Ghana walikasirishwa na kitendo cha mshambuliaji wa timu hiyo ASAMOAH GYAN aliyekosa Penalti dhidi ya Uruguay dakika ya mwisho ambayo ingeweza kuipeleka timu hiyo nusu fainali na kuweka Historia mpya, kwa hasira waliamua kwenda kufanya fujo nyumbani kwa wazazi wa mshambuliaji huyo mjini ACCRA! Sasa mimi najiuliza, si ndie huyuhuyu aliefunga goli la pili dakika za nyongeza na kuipeleka timu iyo robo fainali jamani? ama kweli waswahili kwa kusahau, sasa mama mzazi wa mshambuliaji huyo amempiga marufuku mwanae kutoichezea tena timu kutokana na fujo alizofanyiwa na mashabiki jana...

1 comment:

Anonymous said...

Nikawaida ya mtu mweusi sometimes yes, sometimes no.

Website counter