Saturday, July 3, 2010

TIMU YA TAIFA YA NIGERIA HATARINI KUFUNGIWA NA FIFA...

Baada ya Rais GUDLUCK JONATHAN wa NIGERIA 'pichani', kutangaza kuitoa timu ya yake ya taifa isishiriki katika mashindano yoyote kwa muda wa miaka 2 ili ijipange tena vizuri baada ya kutolewa mapema kwenye hatua ya awali ya Kombe la Dunia linaloendelea hivi sasa, Shirikisho la soka duniani FIFA limetamka kwamba litaifungia timu hiyo kwa muda mrefu zaidi kama agizo la Rais huyu litatekelezwa, kwaiyo imeipa wiki 2 serikali ya nchi hiyo iweze kutengua uamuzi wake! Kwa wale wasiojua ni kwamba FIFA katika katiba yake ina sheria inayosema kwamba Serikali ya nchi yoyote itakayoingilia mchezo wa soka basi inaweza kuifungia isihiriki katika mashindano yoyote timu ya nchi hiyo maana wanaamini Siasa na Soka ni vitu 2 tofauti kama maji na mafuta, umeonaa eeeh...

No comments:

Website counter