Kwangu mimi namwelezea kama mtu makini katika kufanya mambo yake, mcheshi na mwingi wa utani, na hapa namzungumzia Kocha mkuu wa Timu ya Taifa ya TANZANIA anayemaliza muda wake MARCIO MAXIMO! Alikuwa rafiki yangu mkubwa na hasa nilipokuwa nakwenda kufanya nae mahojiano kwa ajili ya vipindi vyangu mbalimbali kwenye TV nilipokuwa home Tanzania. Nakumbuka masihara yake na hadithi zake zilizojaa utani mwingi na ninakumbuka pia jinsi nilivyokuwa namfundisha maneno mengi ya kiswahili cha mtaani na kati ya maneno mengi niliyomfundisha, neno la 'NYUMBA NDOGO' ndio alilolipenda zaidi kiasi kwamba ukipanga naye miadi ya muda kukutana alafu ukachelewa kidogo basi atakwambia umetoka kwenye NYUMBA NDOGO nini, akimaanisha kimada!
Kwa upande wa kikazi pia amejitahidi kwa uwezo wake kutupa somo la kuwa wavumilivu, kuwaamini vijana katika soka, kuwa na misimamo katika maamuzi bila kuyumbishwa! Nimefurahi kwa kuongea nae kwenye simu jana siku aliofanyiwa sherehe ya kuagwa na akaniuliza kama nitakuja tena kumfanyia Interview na nilipomwambia niko nje ya nchi alisikitika sana na kuniambia tuwasiliane kwa email kama atakuwa ameondoka Tanzania! Mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni, kila la kheri MAXIMO na kazi yako tunaojua soka letu la sasa lisilo na wachezaji wenye vipaji maalum TUMEIONA na pia UMETUSOGEZA!
1 comment:
HAPO KAKA BEN TUKO PAMOJA JAMAA NI BONGE LA KOCHA ACHANA NA MANENO YA MITAANI,MIMI MPIRA NIMECHEZA TENA KWA KIWANGO CHA SUPER LEAGUE,NIMECHEZA TUKUYU STAR AND THEN TIGER FC YA TUNDUMA,KOCHA MZURI UTAMJUA JINSI ANAVYOWAELEKEZA WACHEZAJI WAKE JINSI YA KUKABILIANA NA OPPONENTS WAKATI WA MAPUMZIKO BAADA YA KUWA AMESHAONA TIMU YAKE NA OPPONENTS WALIVYOKICHEZA KIPINDI CHA KWANZA,HAPO NDIO KWENYE KIPIMO CHA HARAKA HARAKA UKITAKA KUMSOMA KOCHA,MIMI PIA NIMEWAHI KUONGEA NA MAXIMO JAPO SI RAFIKI YANGU,BALI KWA KUWA MIMI NI MTU WA MPIRA,JAMAA ANAJUA VITU VINGI SANA KUHUSU SOKA,
Post a Comment