Saturday, July 3, 2010

AAAH WABUNGE SASA MNATUUZI BWANAA...


Hii kwangu mimi naona kama kichekesho! Ivi unajua kwamba jana wakati Raisi JAKAYA KIKWETE anarudisha form za kugombea uraisi kule Dodoma eti wabunge wote wa CCM walilikimbia Bunge na kuacha majadiliano yoote ya msingi na kwenda kupiga chabo kwa kikwete wakati anarudisha form pale kwenye viwanja vya Bunge! Unaambiwa Spika alibaki na wabunge 50 tu kati 300 naa, Hiyo inaonyesha jinsi gani watu wasivyo serious na mambo ya msingi ya kutatua kero za wananchi waliowapeleka pale mjengoni, maana Raisi ameenda pale kichama zaidi kurudisha form yake ya ugombea na si ajabu hata yeye kimoyomoyo alijiseme 'hawa nao vipi mbona kiwingu'! Sasa nauliza je akija FREEMAN MBOWE wa CHADEMA kurudisha form si mtatoka mjengoni kuja kuchungulia eeh...

1 comment:

Anonymous said...

yani ben nilizani mi ndo nimeliona hilo hawa watu sometyms sijui wanawaza nini mambo mengine ni yakijinga yanafanya hata vyama pinzani vipate cha kuongea

Website counter