Thursday, September 8, 2011

HEE JAMANI HATA 'NAULI' HUNA, JE USINGENIKUTA...Haa ahaaa maana sina budi kucheka ninapowahadithia kisa hiki wkt nikiwa Bongo wkt natoka kuwatembelea ndugu zangu flani ivi kule Mbezi ila sasa
Wakati nataka kuanza safari ya kurudi zangu home nilikutana na watu wawili; msichana na mvulana wanajibizana. �Yaani hata nauli haunipi, aaah simu yangu haina hata vocha, sasa wakati unaniita ulitegemea mimi fedha ya kujia huku naipata wapi?� ni kauli hii ilitoka kwa mwanamke. Niliwasikia kwa umakini mkubwa, baadaye kwa sababu najuana na mmoja kati yao, niliwafuata, nikajitambulisha, wote wakasema aaah kumbe ndio wewe, nimekuwa nikisoma makala zako kwa zaidi ya miaka kumi sasa, nashukuru sana una ushauri mzuri. Kwa namna walivyokuwa wakizungumza ni kwamba hawakuwa wanajua kama nilikuwa nimesikia namna walivyokuwa wakigombana. Mwanamke anagombania apewe nauli ya kurudi kwao. Ikabidi niwaambie ukweli kuwa niliwasikia walichokuwa wakikizungumza na kwamba sikufurahishwa nacho. Ndipo mwanaume akaanza kusema �Aaah bora umesema, huyu binti bwana ninataka kumuoa, nikamwambia leo kwamba napenda tukutane kwa ajili ya mazungumzo, nashangaa wakati tunaagana analazimisha nimpe nauli wakati mimi mwenyewe kazini hatujalipwa mshahara�. Mikasa ya aina hii ni mingi, kuna wasichana wanaanzisha uhusiano wakiwachukulia wanaume kama mashine za kutolea fedha (ATM). Msichana katoka kwao vizuri, kurudi ni lazima apewe nauli, tena kwa kuomba, hekima iko wapi? Kama una mpango wa kuoana na msichana na anachokiangalia zaidi kwake ni fedha, ni muhimu kupata muda zaidi wa kumchunguza.Kuna wasichana wengine ukiwa naye kwenye daladala yeye ana sh10,000, mwanaume ana sh2000, bado atataka mwanaume ndio alipe nauli.Sijui kosa ni kwanini amemtongoza, huwa sielewi. Kuna wasichana akiwa na mwanaume anamtegeuza mtaji, shida zake zote zitakwisha kwa huyo mwanaume, tena wakati mwingine kwa kulazimisha. Mizinga kwa kila kitu. Eeeh kama uko naye kuanzia chakula, maji, soda na kadhalika, yeye ni mtu wa kula tu, tena wengine wanaweza kukujia hadi na marafiki zake, akukomoe vizuri kwanini umekubali kumpenda. Anakuingiza gharama, wengine unakuta eti hawanywi vinywaji vya bei rahisi. Haya ni maisha ya kipuuzi ambayo ni lazima watu waondokane nayo, maana ya mapenzi ni kusaidiana na kufanyiana mambo ambayo wewe ukifanyiwa utajihisi raha, sio kufanyiana mambo ya kukomoana. Kununuliwa kila kitu ni aibu, kuna wengine wanafanya kazi, lakini fedha zao ni zao na zile za wanaume wao nazo wanataka ziwe zao. Huu ni wizi wa waziwazi. Kama ni suala la kukosa nauli, unapaswa kusema kabla ya kuja. Wasichana wengine ukiwa nao ni matatizo, eeeh kodi ya chumba nilichopanga imekwisha�!!kwa hiyo mwanaume ni ATM? Wakati mwingine huwa sielewi kwanini mwanaume atoe fedha kwa mwanamke, wakati tafiti zinaonyesha hata katika tendo la ngono/ndoa, wanawake ndio wanaopata raha zaidi kuliko wanaume. Unatoa fedha kulipia nini? Ninaowazungumzia hapa ni wale ambao hawako kwenye ndoa, unakuta binti hana kazi ya maana, ana simu ya bei mbaya hata mama yake mzazi hana, hata baba yake mzazi hana, kumbe kamuibia mtu. Je wewe ni kati ya wale ambao kuombwa vocha ni kawaida lakini wanaopigiwa hawajulikani? Ikiwa jibu ndiyo, jua kuwa unaumia. Kivipi? Inawezekana kuna mwingine anayependwa ndiye anapigiwa na wewe unatumikishwa au unaonekana ni pumbavu wa kuibiwa fedha na mali zako. Wapo ambao wanakuwa na sababu za msingi, labda ni kweli anawasiliana na mama yake, labda ni kweli anawasiliana na watu wengine muhimu katika familia yake. Lakini mara nyingi usikubali kuonekana kama ATM. Unaweza kuwa bingwa wa kuhonga, ukifikiri utapendwa, lakini hizo vocha wakatumiwa wengine wanaopendwa. Uwe makini ndugu yangu, achana na vitu visivyo na maana kama hivyo (ngono). Kuna watu wengi wako kibiashara zaidi, ukiwa kwako anasema nakupenda, kumbe kuna watu kama kumi hivi toka asubuhi walishaambiwa nakupenda, usibwete kwa kuamini unapendwa eti kwa sababu umeambiwa. Ni lazima uwe makini na fedha zako. Achana na tabia ya kuhonga, achana na tabia ya ngono, inaongeza umaskini, kwani wasichana wengi kama walivyo wavulana, si waaminifu. Wapo ambao ni waaminifu, ni wachache mno. Ni ujinga pia kumsomesha msichana kwa makubaliano kwamba mtakuja kuoana. Amini ninachokwambia ni nadra sana kuoana naye, zaidi tarajia maumivu. Ni makosa mnapokutana kutoleana ahadi nyingi nzuri. Ni makosa pia unapomkuta mtu kuzungumza juu ya unavyotaka wewe�kwa mfano kuna watu utawakuta wanasema �sitaki Wengi wako kimaslahi zaidi, wako kibiashara zaidi. Ukiwa naye, wako, akitoka tu, ni cha wote�wizi mtupu�fikra ni namna gani naweza kupewa vocha, namna gani naweza kununuliwa chakula cha mchana na mambo mengine yasiyo na maana kama haya. MBINU ZA KUJUA KAMA ANACHOTAKA NI FEDHA AU WEWE; Hebu fanya hivi, kama una msichana ambaye umekuwa ukimtumia vocha, umekuwa ukimsaidia hiki na kile, kuanzia leo hadi mwisho wa wiki hii usimsaidie chochote, halafu uone namna gani atakuwa.
Je unapokuwa hujampa fedha, ukisalimiana naye anaonekanaje? Anakuwa ni mtu wa kuchangamka au anakuwaje hasa? Kwa asilimia kubwa, hata kama labda alikuwa ana kawaida ya kukusalimia kwa kukutumia ujumbe, inakuwa ni mwisho wa salamu hata kama awe na vocha, haki ya Mungu we mjaribu 'DEMU' wa namna hiyo utaona...

No comments:

Website counter