Friday, August 26, 2011

NINAWAKUMBUKA SANA WATU HAWA KWA 'VITUKO' VYAO DAAH...


Huyu ni Beki wa kushoto wa timu ya soka ya SIMBA na Taifa Starz aitwae AMIR MAFTAH. Ni rafiki yangu mkubwa na ambaye kuna baadhi ya 'MAMBO na VITUKO' vyake nikivikumbuka huwa nacheka Peke yangu, sasa ngoja nikwambie ninayoyakumbuka kutoka kwake, ni kwamba huyu jamaa kama ukikutana nae kwa maongezi ni lazima uwe makini sana kumsikiliza maana anaongea kwa 'KASI' sana na kwa mtiririko wa hali ya juu bila kukosea maneno au 'Points' zake! Anaweza kuwa ni miongozi mwa watu wanaongea kwa kasi na haraka zaidi nchini endapo kutatokea 'SHINDANO' la aina hiyo...

Huyu anaitwa PETER MANYIKA, ni Golikipa maarufu wa zamani wa Yanga na Taifa starz ambaye kwasasa ni Kocha wa makipa wa Timu ya Taifa ya Vijana U23! ni rafiki yangu pia na kuna baadhi ya Mambo nayakumbuka kutoka kwake na haswa unapoongea nae 'Ana kwa Ana' huwa 'HAKUANGALII KABSAA USONI' labda ulazimishe akuangalie, sasa sijui siku akienda kwenye 'INTAVIUU' sehemu itakuwaje maana inaelekea tayari ni 'Kilema' wa Jambo hilo...

Huyu ni aliyekuwa Rapa Hodari wa Twanga Pepeta SAULO JOHN aka 'FERGUSON' ambaye kwasasa anapiga 'mzigo' ndani ya Bendi ya EXTRA BONGO aka 'Wazee wa vizigo' inayoongozwa na ALLY CHOKI 'mzee wa Farasi'. Picha hii nilimpiga wkt wa Harusi yake na mchumba wake wa sikunyingi ANGEL BUSHOKE ambapo mie pia ndie niliyekuwa MC wa Harusi hiyo! Nae ni swahiba wangu ila nawaambieni na mniamini, Jamaa ana kipaji Kikubwa cha 'UCHEKESHAJI' amini usiamini, yaani huwa najiuliza ni kwanini anaacha kipaji hiki cha kuchekesha kipotee ingawa amezama kwenye Muziki! Kama huamini kwa wale wanaofahamiana nae watakuwa mashaidi, we kakae na jamaa kwa muda mfupi alafu uone 'MBAVU' zako kama zitasalimika...

Na huyu sasa ni Waziri wetu MKUU wa Tanzania Mh. MIZENGO KAYANZA PINDA! Nae ni swahiba wangu vilevile ingawa ana vituko vingi huwezi kudhania! Mara ya mwisho nilikutana nae nyumbani kwake mjini Dodoma ambapo katika maongezi yetu baada ya 'Dinner' alianza kunisimulia kuhusu 'MIFUGO' yake anayofuga kijijini kwake kule Mpanda RUKWA, basi kila nibadili 'Topic' yeye anabadilisha aina za wanyama tu, alianza kuhusu 'NG'OMBE' mara akahamia kuhusu ufugaji wake wa 'NYUKI', basi daa mie ni kicheko tu wkt yeye mwenyewe alikuwa 'SIRIAZI' kishenzi na kujisifia! Kwa hakika namkumbuka mzee huyu kwa kupenda KILIMO na UFUGAJI ...

No comments:

Website counter