Tuesday, August 30, 2011

MSIKIENI HUYU 'ALIYENASA' KWENYE PENZI LA BABA MKWE WAKE LOOH...


KILA atakayesoma maelezo haya ataniona mimi ni mjinga kutokana na jinsi nilivyonasa katika penzi la baba mkwe. Jina langu ni Pili, ni mkazi wa jiji la Dar es Salam nimekutana na mkasa ambao kwa kweli siwezi hata kujinasua.

Kisa na mkasa ni simu, kwani siku moja nilipokea Ujumbe Mfupi wa Maneno (SMS) wa mahaba ukinisifia kwa kiwango cha juu jinsi nilivyoumbika.

Pamoja na kuwa na mume wangu wa ndoa, lakini hata siku moja hajathubutu
kunisifia kwamba nimeumbika, nikashangaa kusifiwa tena na mtu nisiyemjua.

Niliipenda SMS ile na kuijibu kwa kushukuru kwa kusifiwa lakini kuna kitu kimoja sikukielewa kama ujumbe ule ulikuwa ‘umenuiziwa’ maneno ya mahaba nyuma yake, kwani nilipomaliza kuusoma, mwili wangu ulisisimka na kutamani kumjua aliyenitumia.

Niliendelea kuchati na mwanaume yule bila ya kumjua, naye akawa anaendeleza kunimwagia SMS za mapenzi yaliyopitiliza.
Ghafla nilijisikia mwenye furaha moyoni kumpata mwanamume mwenye kuonesha mapenzi ya dhati kwangu.

Nilimuuliza jina lake naye alinitajia lakini bado sikumfahamu. Tuliendelea kuchati mara kwa mara na hakika mwanaume alikuwa ni mtaalam sana wa maneno ya mahaba.

Wakati mwingine nilijikuta nikimaliza haja zangu kutokana na maneno yake yaliyokuwa yamejaa hamasa za mapenzi za hali ya juu.

Niliongeza upendo kwake na kumuona mume kuwa si mali kitu. Hilo lilichangiwa na uchovu wa mume kushindwa kunisifia na uchovu wake katika uwanja wa fundi seremala kwani alikuwa si lolote wala si chochote.

Siku moja tulipanga kukutana na mwanamume yule niliyekuwa nikichati naye, ndipo nilipojikuta nimeangukia mikononi mwa baba mkwe wangu, yaani baba wa mume wangu.


Sikuamini macho yangu, nilitaka kukimbia, lakini yeye akaniambia kuwa sikuwa na haja ya kukimbia, kama dhambi ya uzinzi tayari tumeshaifanya kwa kuchati kwenye simu, kilichobaki tuanzie pale tulipoishia.

Nilifikiria sana, kwa kuwa sikuwa na dhamira ya kutenda tendo na baba mkwe, wakati najiuliza, baba mkwe alinisolea na akanishika mkono, ghafla mwili wangu ulisisimka kwa raha ya mahaba isiyokuwa na kifani na mwili wangu ukalegea.

Ghafla nilipata ujasiri wa ajabu wa kuisaliti ndoa yangu tena na baba mkwe. Nikiwa nafurahia penzi la baba mkwe mwaka mmoja ukapita, Mungu alimwita mume wangu mbele ya haki na kuniacha nikitanua na baba yake mpaka sasa.

Basi mpaka sasa bado nimenasa katika penzi la baba mkwe, sijui jinsi ya kujinasua, nakumbuka kuwa chanzo kilikuwa ni SMS tu. Sijui nitajinasuaje...

4 comments:

Anonymous said...

mmh! we ni malaya tu usituulze ujinga wako

Anonymous said...

Pumbavuuuuuuuuuuuuu ndo maneno ya kutueleza huna akili hata kidogo,achana na baba mkwe wako haraka

Anonymous said...

Wewe ni mshenzi na ndo umeshirikiana na huyo hayawani mwenzio kumuua mumeo, hii dhambi uliyofanya na unayoendelea kuifanya subiri mvua ya laana ikianza kukunyeshea utakiona cha mtema kuni!

Anonymous said...

hakika ni laana ya dunia mpaka akheraa!!! nyie wote ni wa motoni tu msonyo mreeeeeefuuuuuu.....!

Website counter