Sunday, August 21, 2011


Anaitwa ANDREW ALEXANDER COLE lakini wengi tumezoea kumuita ANDY COLE! Ni mshambuliaji Hatari wa zamani wa Mashetani Wekundu 'MAN UTD' ambaye daima ushirikiano wake uwanjani na mshambuliaji mwenzie PACHA raia wa Trindad And Tobacco DWIGHT YORKE ulifanya Dunia 'kutikisika' kwa kila timu inayokutana na Manchester United uwanjani kwa ukali wao wa 'kuzifumania' NYAVU!

Alizaliwa tar 15 oct 1971 mjini Nottingham nchini Uwingereza. Mshambuliaji huyu mweusi ameshafunga magoli 187 katika Ligi ya soka ya England akishika nafasi ya pili nyuma ya 'Nguli' ALAIN SHEARER anayeongoza kwa kufunga magoli 260! Kwasasa ni Kocha wa Washambuliaji wa timu ya HUDDERSFIELDS liyoko ligi daraja la kwanza nchini humo na alistaafu kucheza soka la Ushindani mnamo tar 11 nov 2008. COLE amemuoa 'Demu' wake wa sikunyingi SHIRLEY DEWAR mwezi Julai 2002 ambayo pia siku hiyo Winga hatari wa zamani wa Liverpool STEVE MAc MANAMAN nae alikuwa anaoa! Huyu bwana anaishi eneo la North West ambako jirani yake mkubwa ni Beki 'KISIKI' wa Man Utd RIO FERDINAND...

No comments:

Website counter