Saturday, July 30, 2011

HII NDIO MADA YA LEO, TUIJADILI...


Unapompigia mtu simu hapokei, kuna ulazima kuendelea kupiga? Send to a friend


SIMU ni kiunganishi ambacho wengi wanakitumia kwa ajili ya mambo mbalimbali hasa katika upande wa mawasiliano. Lakini simu imekuwa ni sababu kubwa ya wengi kutofautiana hasa, wanaodaiana na hata wanandoa. Lakini lililopo mezani leo ni hili. Unapompigia simu mtu na kisha ukaona kwamba hapokei simu yako unahisi nini, na je? Kuna ulazima wa kuendelea kumpigia?

Mary Misoji Ng'oboko
Ukweli ni kwamba mtu akikupigia simu mara nyingi anaudhi, kwa upande wangu huwa sipendi kabisa mambo kama haya. Sasa kama anaona mtu hapokei kuna ulazima wa kuendelea kumpigia?

Annamiriam Mgonja
Duh, huyo ana moyo. Mie mara moja tu kama hupokei sipigi tena

Man Jah
Hauwezi jua umuhimu wake labda mpenzi wake ndio maana anapiga mara nyingi sababu ana hamu ya kuongea naye.

Mwandu Michael
Mi naona huyo mtu anatafutwa kwa utapeli alioufanya! Na ndio maana hataki kupokea kwani ni vema kupokea simu kwani huwezi jua huyo mtu amepatwa na tatizo gani.

Ashraf Omar
Hapana mimi napinga, kwani kuna siku nilikuta missed call 57...42 za mtu mmoja jamani kama anaona sipokei ajue nipo mbali na simu.

Gerald Ndokole
Anaweza kuwa mpenzi wake na anaamini yupo na mtu mwingine faragha, si mnajua jamani wivu ulivyo, atakuta na hiyo simu kaipasua ukutani!!

Adriano Dominic
We upokee tu umsikilizie, kwani huwezi jua mtu ana matatizo gani, wakati mwingine watu tunakosea baadhi ya mambo.

Rhobin Chriss
Du! Lakini si unajua mbio za panya hazina mshindi kwani hata ukishnda bado utabaki panya tu kwahiyo labda anafukuzia deni lake.

Botully Ali
Labda kuna dharura si vizuri kupuuza baadae anaweza juta.

Marylne Felix
Kwan unapopiga simu mtu hapokei ina maana hayupo karibu na simu au yupo sehemu ambayo hawezi kuongea vazuri na wewe au hataki kupokea simu yako hivyo unachotakiwa kufanya ni kuacha kama anataka kuwasiliana na wewe atakupigia, kupiga simu ya mtu mara 17 ni ushamba!

Gerald Ndokole
Hiyo ni simu ya mkononi, kuacha na kwenda kuzurura pia ni ushamba!

Swalehe Atway
Huyo mwenye cm huwenda hakawa hajielewi, kama upo sehemu faragha zima simu, unajua kabisa simu huwezi kupokea unaacha simu hewan sisi wa Afrika tunaishi kufuatana na Kantian Ethic's,wakat mwingine huwenda kuna tatizo au unatafutwa na polisi au kuna msiba unataka kutaarifiwa unapuuzia.

Frank Mkocha
Kama kuna sababu ya msingi ya kupiga utaendelea kupiga hadi ipokelewe la sivyo utampotezea

Yahya Ramadhan
Hawako sawa wote hao, we kwanini upige mara zote hizo kama haipokelewi? nawe kwanini hupokei au ushamba tu?

Yahya Ramadhan
Wanalao jambo sio bure.

Godwill Akilimali
Wengine wanakuwa na shida ya muhimu.

Sam Mujinja
Ukimpigia mtu simu mara kibao hapokei ndio maana ikawekwa facilities ya short message, mwingine anaweza kuwa kwa kikao, ama kwenye kuwasilisha mada, unapoendelea kumpigia unamsumbua zaidi,ukiona hapokei tuma massage. Kama hajajibu basi.

Charles Kalambo
Simu ya mkononi ina maana yake bila hivyo tungekuwa tunaziacha nyumbani tukaenda maofisini.

No comments:

Website counter