Friday, May 6, 2011

NAJIULIZA SIJUI NIJITOSE 'KUSULUHISHA' UGOMVI HUU, MAANA NAONA 'MWISHO' WAKE MBAYA, AU AU 'NIJIKALIE' ZANGU PEMBENI...MSANII maarufu wa filamu nchini, Wema Sepetu, pichani, amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Mwanzo Kinondoni mkoani Dar es salaam akikabiliwa na mashitaka ya kumtukana Raheem Rummy ambaye anatajwa kuwa ni Rais wa kundi la Masharobaro.Wema (26) ambaye ni Miss Tanzania mwaka 2006 na pia ni mwigizaji mahiri alifikishwa mahakamani hapo jana na kusomewa mashitaka mbele ya Hakimu Mfawidhi Mariam Masamalo.Msanii huyo ambaye hadi gazeti hili linaondoka mahakamani hapo mchana alikuwa hajapata dhamana alisindikizwa na baadhi ya wasanii wenzake akiwemo mwigizaji Rose Ndauka.Karani Sharifa Dunia, alidai mbele ya Hakimu Masamalo kuwa, Aprili 11,mwaka huu saa 12.38 jioni huko Kinondoni mshitakiwa alimtukana Rummy matusi ya nguoni.Wema alikiri kutukana matusi hayo baada ya kuulizwa na hakimu Mariamu kama mashitaka aliyosomewa ni kweli au si kweli.“Ni kweli nimemtukana lakini ilikuwa hasira tu,”alijibu Wema baada ya Hakimu Mariam kumuuliza sababu za yeye kutukana matusi hayo.Kesi itatajwa tena Mei 18 mwaka huu kwa ajili ya kusomewa maelezo ya awali na mshitakiwa yupo nje kwa dhamana baada ya kutimiza masharti ya dhamana.

Miezi kadhaa iliyopita msichana huyo alipandishwa kizimbani katika Mahakama ya Kisutu, Dar es Salaam kujibu mashitaka ya kuharibu gari la aliyekuwa mpenzi wake, Stephen Kanumba.

No comments:

Website counter