Monday, May 16, 2011

KWENYE KONA YA MAHABA LEO HII 'NAKUJUZA' DALILI 5 ZA KUMTAMBUA MUME ANAYETEMBEA NA 'HAUSIGELI'...
Aaah mie wiki hii bwana nataka kuingia kidogo kwa wanandoa! Nazungumzia wanandoa, yaani wale walio katika maagano ya maisha, kwamba wamepita kanisani, msikitini wakaoana.

Lakini si mbaya hata kwa wale ambao hawajapita huko, lakini wamejenga familia inayokubalika.
Familia nyingi siku hizi zina majukumu mengi na ili kupunguza hali hiyo, wanaajiri wasichana wa kazi ambayo zamani walikuwa wanajulikana sana kwa jina la ‘yaya’.
Siku hizi, ama wao wenyewe au waajiri wao wamefanya mageuzi na kuwaita house girl au ‘hausigeli’.

Hali iliyopo sasa ni vilio. Wanawake wengi wamekuwa wakilizwa na mahausigeli kwa kutembea na waume zao. Naamini wewe msomaji, kama hakuna nduguyo aliyewahi kukumbwa na janga hili la mumewe kula ‘vyombo’ vya hausigeli basi rafiki au jirani.
Kinachoonekana siku hizi ni kuwa, mahausigeli wenyewe wamejua udhaifu wa wanawake kwenye ndoa. Na wao wanatumia nafasi hiyo kutuliza mpira kifuani, halafu mguuni na kupiga bao.

KIINI CHA TATIZO.
Kwanza, kabla sijaanza kuanika Dalili 5 za Kumtambua Mume Anayetembea na Hausigeli, ni vyema niwajulishe kiini cha tatizo.
Zamani, msichana wa kazi alikuwa na mipaka ndani ya nyumba.

Mfano, alikuwa hawezi kufua nguo za mwanaume. Nguo zake ni za watoto, kidogo na za mama mwenye nyumba. Siku hizi, wasichana wa kazi wanafua suruali, bukta, pensi, soksi, singilendi za baba! Mbaya sana.
Nguo kama singilendi, ni sawa na ‘kufuli’ la ndani. Kwani matumizi yake yanafanana, baba hawezi kuvaa shati mpaka aanze na singilendi, ni kama asivyoweza kuvaa suruali mpaka aanze na kufuli.

MAMBO HUANZA HAPA.
Sasa wewe mke unapompa hausigeli nguo za mumeo ili azifue unataka nini? Atafua, ataanua, atazikunja na kuziingiza ndani. Baba atavaa akijua kafua hausigeli, kama zilitakata sana si atamsifia yeye! Wewe una chako hapo?

Kingine, wake za watu siku hizi bwana hawataki shida kama wale wa zamani. Siku hizi, utamkuta mama amekaa sebuleni anaangalia tamthiliya ya Don’t Mess With Angel huku hausigeli akimpikia mzee. Na ikitokea mzee akachelewa kurudi, anamwambia msichana asilale asubiri kumfungulia mlango mumewe, wenyewe wanaita baba. Yeye anakwenda kujitupa kitandani.

Mzee anaporudi anakutana na hausigeli, ndiye anayemkaribisha na kumpa pole kwa kazi. Baba anaitika asante dada. Anakaa kwenye kochi, anavua viatu. Msichana anachukua soksi na viatu na kuavipeleka mahali pake.
Baada ya hapo, anamkaribisha baba kwa ajili ya chakula. Huwa inakuwa hivi:
Hausigeli: Baba karibu chakula.

Baba: (huku ananawa) haya asante, kuna ndimu?
Hausigeli: Ngoja nikakuletee.
Wakati anaondoka, baba si katoka kazini, macho yake yanataka kubadili aina ya mambo aliyoyaona kazini, lazima atamwangalia msichana kwa nyuma.
Ikitokea msichana kaumbwa, akaumbika. Baba anaguna!

Baba: Mh!
Asubuhi kukicha, baba akiamka, mtu wa kwanza kukutana naye nje msichana wa kazi. Watasalimiana kisha msichana atamwambia ‘baba maji ya kuoga tayari’ wewe mama bado upo kitandani.

Baba akishaoga, atavaa, atakwenda kukaa sebuleni kwa ajili ya kunywa chai. Dada ndiye atakayepita pita akiendelea na shughuli zake. Mwishowe, atakuja kukuaga wewe chumbani, akitoka atamalizia na dada.

Hali hii itaendelea hadi baba atakuja kuingia majaribuni kwa sababu amekuwa huru sana na msichana wa kazi za ndani, anakuwa naye kwa muda mrefu kuliko mkewe na ndiye anayempa huduma zaidi.

Mara nyingi sana, huwa inafika mahali, mume akiwa anataka kitu, mfano ‘sendoz’, hata kama wewe upo, yeye anaita ‘dada’.
Hausigeli: Abee.
Baba: Niletee sendoz zangu nyeusi.
Wewe mke upo na wala hujisikii kama unapigwa bao pole pole. Mh! Kalaghabaho.

3 comments:

Anonymous said...

Ww nawe punguza story zenye ujumbe mrefu kama barua ...kuwa. up 2 date NA mambo mazuri NA yenye ujumbe mfupi

Majoy said...

nzuri sana hii thanx Ben ni kweli wanawake siku hizi tunajisahau sana.wakati umefika sasa wamama tuhudumie waume zetu tusiwaachie ma house maid.

Anonymous said...

he he he hapo umetupa ushauri mzuri sanaa,tuliokuwa kwenye ndoa,ni vitu ambavyo vinatokea kabisaa,na wanandoa tunatakiwa kuwajari waume zetu,sio kuwaachia housegirls wawaangalie waume zetu,huo ni ujinga,.
By Grace Helgesen!

Website counter