Thursday, May 12, 2011

JUZI KATI NILIPOWAKUSANYA 'RAFIKI' ZANGU KWENYE MECHI YA MCHANGANI...


Juzi jioni kulikuwa na mechi ya Kirafiki ya 'MCHANGANI' ya kujifurahisha kati ya Timu yetu ya Mtaa ya NATIONAL ya kwetu Kinondoni na 'SWAHIBA' zangu wa Timu ya wachezaji wa zamani na wa sasa ya 'DAR ALL STARZ' inayoongozwa na ATHUMANI TIPPO iliyofanyika katika uwanja wa GARDEN ulioko Kinondoni jijini Dar na matokeo yakawa 'BILA BILA! Sasa cha ajabu ni kwamba makipa wetu wote Bora nchini wanaodakia Timu ya Taifa, yaani JUMA KASEJA kushoto mwa hii picha na SHAABAN KADO alievua shati wooote walicheza ndani kama washambuliaji na walionesha kiwango kizuri ambacho mashabiki waliohudhuria mechi hiyo 'WALISTAAJABU SANAAA! Picha hii ni mara baada ya mechi hiyo ambayo mimi pamoja na Bw. ATHUMAN TIPPO aliyevaa kanzu kulia, ambaye ni kiungo wa zamani wa COSTAL UNION ya Tanga ndio tuliyoiandaa mechi hiyo kali AJABU!

We mchec uyo SHAABAN KADO pichani kulia alivyovaa, hutaamini kwamba ni 'Golikipa' tena wa kutegemewa wa Timu ya soka ya Taifa, TAIFA STARZ daah! Kushoto aliyeinama ni Mshambuliaji machachari wa timu ya wekundu wa Msimbazi SIMBA ya jijini MUSA HASSAN aka 'Mgosi'...

Na hapa mchec huyo JUMA KASEJA nae alivyovaa, utadhani sio kipa Namba MOKO wa SIMBA na Timu ya Taifa duuh...

No comments:

Website counter