Thursday, May 19, 2011


Anaitwa ZINEDINE YAZID ZIDANE aka "ZIZOU", Ni mmoja kati ya wanasoka wachache mahiri kuwahi kutokea Duniani. Ni kiungo mahiri wa Kifaransa mwenye asili ya Algeria aliyezaliwa Tar 23 june 1972 mjini Marseille nchini Ufaransa kutoka kwa wazazi 'WAZAMIAJI' kutoka Algeria Bw. ISMAIL na MALIKA ambao walihamia Ufaransa wakitokea katika kijiji cha AGUEMONE uko KABYLIE nchini Algeria!

ZIDANE ameoa na alikutana na mkeo VERONIQ FERNANDEZ wakati akiichezea Timu ya CANNES mwaka 1988 na wamejaaliwa kuwa na watoto wa 4 ambao ni ENZO ZIDANE, LUCA ZIDANE, THEO ZIDANE ambao woote ni wacheza soka wanaochipukia na wapo kwenye Timu ya watoto ya REAL MADRID kwasasa na wa mwisho ni ELYAZ!

Jamaa ni mvutaji mzuri wa 'SIGARA' ingawa huwezi kumkuta kivuta 'Hadharani' hata siku moja ikiwa ni moja ya 'kanuni' zake alizojiwekea...

No comments:

Website counter