Sunday, April 24, 2011

SIKIA 'NDOTO' ZA MAPACHA HAWA WA NIGERIA...


MAPACHA wanaotamba kwenye filamu za Nigeria, Chidinma na Chidiebere Aneke wanatamani kuolewa na wanaume mapacha na wazae mapacha kama wao. Wasanii hao wa kike wamesema: �'Tunatamani tukiolewa tuzae mapacha wa aina mbili, wawili wa kike na wawili wa kiume na tuishi kwa amani na waume zetu.� �Tunatamani pia kuolewa siku moja wote wawili, na ikiwezekana na wanaume ambao ni mapacha kama sisi. Lakini tuna imani Mungu atatuchagulia wanaume wanaotufaa. Hatutaki sana kujadili maisha yetu binafsi lakini kifupi ni kwamba tunaishi kwa raha sana na mambo mengine ni siri sana hatuwezi kuyasema'.�

No comments:

Website counter