Sunday, April 10, 2011

JE WAJUA 'MMILIKI' WA TP MAZEMBE ALIKUWA MUUZA SAMAKI?....


Anaitwa MOISE KATUMBI CHAPWE! Ndie mmiliki wa Club bingwa ya Soka barani Africa TP MAZEMBE iliyoifunga SIMBA juzi hapa Dar na ni mmoja kati ya watu 'matajiri' sana nchini CONGO DRC ambaye pia ni GAvana wa jimbo la KATANGA kule kwao Congo aliyezaliwa Tar 28 dec 1964! Ni mdogo kiumri ila ana utajiri wa kutisha kiasi kwamba kama ni Barabara kwenye Jimbo lake anatengeneza mwenyewe bila pesa ya Serikali, anajenga Mahospital mwenyewe na ana majumba mengi ya Disco ya kustarehe na kila siku nje ya 'GETI' la nyumbani kwake kuna 'OMBAOMBA' wanaojipanga msururu wa kuomba pesa ya Chai nae bila hiyana anawapa! Anaheshimika kama 'MUNGU' kule na ukitaka 'KIFO' nenda pale Lubumbashi alafu simama sehemu yoyote mtaani kisha anza kutoa maneno ya 'kumkashifu' mtu huyu alafu uone utakachofanywa na wananchi walio pembeni yako! Ila wajua kwamba jamaa alikuwa anauza SAMAKI tangu akiwa na umri wa miaka 12? Na faida yake ya kwanza ni dola 40 tu ambayo ni kama 60,000 ya kibongo lakini leo hii anamiliki machimbo makubwa ya Dhahabu na ALMASI. Ana kaka yake mkubwa aitwae RHAPAEL KATOTO CHAPWE ambaye anaishi BELGIUM anayesema kwa 'kebehi' kwamba kwa wale woote wanaomwona MOISE eti ndio tajiri kwenye Familia yao basi wamekosea maana 'MOISE ndio mtu masikini zaidi katika Familia yetu' anasema Raphael. Hapo ndio utajua jinsi gani 'WAKONGO' wanavyopenda sifa na kujipamba, HABARI NDIO HIYOO....

No comments:

Website counter