Hemed |
MSANII anayewika katika tasnia ya filamu Hemedi Seif a.k.a PHD (Pretty Huge Dude) kwa kushirikiana na Yusufu Mlela wameandaa ambayo itaanza kurekodiwa mwezi ujao.
Hii imekuja baada ya muda mrefu wa malumbano baina yao hali iliyofikia wakatwangana ngumi �live� bila chenga.
Hemed ambaye alitikisa katika muziki wa kizazi kipya baada ya kung�ara zaidi kupitia shindano la Tusker Project Fame anesema, projecti hiyo itatambulika kwa jina la Msitu.
�Katika kuhakikisha tunapiga makasia kwenye tasnia ya filamu tumeshirikiana na Yusufu Mlela kuandaa huo Msitu ambao mzigo wake utaanza kupigwa Februari 12,� alisema Hemedi.
Aidha Hemed anasema ameandaa filamu zake mbili ambazo ni The Sound Death na Life ambazo pia zitaingia sokoni mwezi Februari.
Kwa mujibu wa Hemed filamu ya The Sound Death imerekodiwa naa Game first quality na Life imefanyika chini ya Bajomba Production
No comments:
Post a Comment