Sunday, March 6, 2011

'A TO Z' YA MECHI YA JANA KATI YA WATANI WA JADI NCHINI SIMBA NA YANGA...


Wachezaji wa Timu zote wakijiandaa kuingia uwanjani tayari mkuuanzisha MTANANGE huo wa watani wa jadi jana...

Nikiwa na rafiki zangu ambao ndio Manahodha wa timu hizo za watani wa jadi SIMBA na YANGA, katikati ni MUSSA HASSAN 'MGOSI' wa SIMBA ambaye pia ndie mfungaji wa jana wa Goli la Simba na kulia ni SHADRAQ NSAJIGWA 'FUSO' wa YANGA...

Huwa napenda kuwapa 'SAPOTI' watu wangu woote wa karibu wanapofanya kazi zao kama wao wanavyofanya kwangu, hapa nikiwa Swahiba zangu kushoto ni OTHMAN IDDI 'CHUJI' na kulia ni FRED MBUNA ambaye ndie mchezaji mzee kuliko woote wa YANGA kwasasa...

Nikijadiliana jambo na Mshkaji wangu Golikipa wa Simba JUMA KASEJA baada ya JERRY TEGETE wa Yanga 'kumkosakosa' dakika za mwishoni mwa mchezo huo uliofanyika jana kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar...

Kati ya Mabeki wagumu nchini wanaocheza 'JIHAD' basi 'Mzenj' huyu NADIR HAROUB Cannavaro ambaye ni Beki 'kisiki' wa YANGA na Taifa Starz anaongoza, ila ni mtu mpole sana anapokuwa nje ya Uwanja na usiku huu amenipigia simu kuniambia kwamba Mguu wake wa kulia 'unamuuma' baada ya kuumia kwenye mechi ya jana na amelala 'HOI' kitandani ila kesho jioni ameniomba tutoke twende 'LEADERZ CLUB' Kinondoni wanakopiga TWANGA PEPETA...

No comments:

Website counter