Sunday, March 20, 2011

HUYU NI RAFIKI YANGU WA UKWELI NAOMBA TUMSAIDIE KUMNUNULIA 'BAISKELI' JAM ANI...


Huyu ni rafiki yangu wa ukweli kabisaa, anaitwa GODFREY na ana umri wa miaka 28 sasa ingawa ni 'MLEMAVU WA VIUNGO' na ni mwenyeji wa mkoa wa SINGIDA! Ni shabiki wangu mkubwa sana na kila akinionaga huwa anafurahi sana ila maskini hawezi kufanya kazi yoyote kutokana na maumbile yake! Anaishi kwa msamaria mwema mmoja pale UPANGA na mwenyewe anasema anayakubali maumbile yake na anamshukuru mungu yoote aliyompa ila kinachoniuma ni kwamba hana hata Kibaskeli cha kutembelea na maranyingi nikimtembeleaga huwa anatumia kama nusu saa kutoka nje na kunifikia mlangoni kwani huwa 'ANAJIBURUTA' mwenyewe kwenye 'VUMBI' na kwakweli nimeamua kuanzisha 'Harambee' ya kuchanga Pesa za kumsaidia rafiki yetu huyu kumnunulia kile 'Kibaskeli' cha kutembelea walemavu maana hakupenda kuumbwa hivyo alivyo! Jiulize na kujirudi jamani, mbona kwenye HARUSI mnachanga mipesa kibao jamani...

Kumbukeni pamoja na kuwa ni 'MLEMAVU WA VIUNGO' lakini ni mtu mzima mwenye kuelewa anachosema maana ana miaka 28 sasa na kwa hakika ukimsikiliza utagundua ni mtu mwenye akili sana ila ndio ivyo tena maisha yamekuwa ivyo! Jamani wenye imani ya kumsaidia GODFREY naomba tuwasiliane kwa chochote kuanzia 'PESA' za Harambee ya kudunduliza ili tumnunulie 'BAISKELI' ya kutembelea na hata Nguo haswa zile kama za watoto wa umri wa miaka 5 nadhani zitamtosha na kutoa ni moyo na BARAKA! mawasiliano yangu ni +255 655 705 055. Au kwa email- bennytanzania@yahoo.com

No comments:

Website counter