Friday, February 11, 2011


Huyu ni KHADIJA MNOGA aka 'Kimobitel' ambaye ni muimbaji wa zamani wa Twanga Pepeta aliyeamua kurudi kundini kutoka Bendi ya Extra Bongo ya ALLY CHOKI baada ya 'kuhitlafiana' kwa mambo anayoyajua mwenyewe maana nilijaribi kumuuliza kwanini ameamua kurudi Twanga aah nikaona ananitolea macho 2! Ni mwimbaji mwenye wapenzi wengi na mahiri...

'KIMOBITEL' akimba na wana Twanga Pepeta kwa mara ya kwanza jana ndani ya ukumbi wa BILICANAZ CLUB...

Huyu ni GREYSON SEMSEKWA, ni Rapa ambaye pia alikuwa katika bendi ya Extra Bongo ya mzee wa Farasi ALLY CHOKI, nae ameamua kujiunga na Twanga Pepeta kuanzia jana! Ni rapa mbaye alishawahi kufanyiwa 'Operation' ya Koo na sasa yuko Fit na sauti pia inatoka kwa ubora wake wa kawaida, ni Rapa mbunifu sana ambaye anaweza kutunga rap muda wowote na wakati wowote...

SEMSEKWA akighani jana kwa mara ya kwanza na wana TWANGA PEPETA...

No comments:

Website counter