Friday, February 18, 2011

'CHAMA' JIPYA LA 'MAANGAMIZI' LAZINDULIWA DAR...


Jamani habari mpya ni kwamba tumeanzisha timu kali ya 'KUTISHA' inayoundwa na wasanii wa Bongo Flava na Watangazaji ambayo mpaka naongea hivi sasa tumeshacheza mechi 2 za kujipima nguvu na tumeshinda 1 na tumetoa Droo 1. Na kwasasa kuna baadhi ya Makampuni yamejitokeza kutaka kutusaidia kutupa Udhamini ili Timu yetu iendelee kwenda 'Ki Profeshino' zaidi. kwenye hii picha ni mechi ya Juzi kati yetu na Timu ya Kombaini ya mkoa wa Dar es salaam inayoundwa na wachezaji kibao wa zamani na wa sasa kutoka Ligi kuu Tanzania bara na hatimae 'tukagangamala' na kutoka nao Droo ya baao 3 - 3 na mie nikatumbukiza bao 1 kati ya hayo matatu kudaadeekiii. Baadhi ya wachezaji wanaunda timu yetu ya wasanii na watangazaji ni Mimi mwenyewe 'STRAIKA' BEN KINYAIYA, wanamuziki ALLY KIBA, H. BABA, LUTENI KARAMA, BUSHOKE, KR MULLA, CHEGGE, MH. TEMBA, RICH ONE, MAKAMUA, SHAFFII DAUDA na wengineo kibao, na kama huamini kuna Bonge la 'Game' linakuja kati yetu na Timu ya wacheza FILAMU Tanzania wakiongozwa na kina RAY, KANUMBA DK CHENI, CHECBUD HEMED, YUSSUPH MLELA na wengineo kibao kwa udhamini wa kampuni flani ivi staki kuitaja maana ni mapema kuisema sasaivi, sio ya KUKOSA!

Hapo kuanzia kushoto ni wanamuziki wa Bongo Flava ALLY KIBA na katikati ni H. BABA tukipanga mipango kabla ya Game kuanza, ni Haatwaariii nakwambia...

Hiki ni kikosi chetu kizima cha MAANGAMIZI kilichotoka Droo na Kombaini ya mkoa wa Dar juzi kwenye kiwanJa cha Ustawi wa Jamii Kijitonyama...

No comments:

Website counter