Wednesday, January 5, 2011

UMEISKIA HII, KUANZIA SASA MAJINA YA 'KINGEREZA' SASA MARUFUKU KWENYE FILAMU ZA KIBONGO DAAH...




BODI ya Ukaguzi wa Filamu imepiga marufuku filamu za Kiswahili kutumia majina ya Kingereza kwenye filamu zae kama ambavyo imekidhiri.

Onyo hilo limetolewa na Katibu Mkuu wa Bodi ya Filamu nchini, Joyce Fisso wakati akiongea na wasambazaji wa filamu hizo katika ukumbi wa mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam hivi karibuni

“Kisheria si ruhusa kutumia majina ya lugha ya Kiingereza au lugha nyingine tofauti na ile ya Kiswahili ambayo ndiyo lugha ya taifa, kama kuna mtayarishaji ambaye ataona kuna umuhimu wa kutumia lugha nyingine tofauti na lugha yetu ya Taifa, anatakiwa kuandika jina hilo kwa herufi ndogo kwenye mabano,”alisema Fisso.

Alisema watayarishaji wengi pamoja na wasanii wamekuwa hawajui kuhusu taratibu hizo ambazo zipo kisheria kwa sababu hiyo filamu nyingi zimekuwa zikitolewa kiholela bila kukaguliwa na bodi yake kuanzia utayarishaji wa awali, ukaguzi wa mswada pamoja na bajeti kwani baada ya kukamilisha hayo bodi hutoa kibali kwa ajili ya utengenezaji wa filamu.

"Majukumu ya bodi yapo wazi ni wajibu kila mtayarishaji awajibike kufuata taratibu za bodi Bodi ya Ukaguzi wa Filamu na Michezo ya Kuigiza mwaka huu mpya ni lazima tuhakiksihe filamu na michezo ya kuigiza inawajibika na kuwiana na mila, desturi na maadili mema ya Tanzania.

Pia, na kuhakikisha upangaji wa madaraja ya maonyesho ya filamu na michezo ya kuigiza unalingana na mabadiliko ya maadili mema ya jamii ya Watanzania.

"Tutahakikisha pia usanii na uhuru wa ubunifu wa sanaa hauzuiliwi bila sababu za msingi, na inakuwa kwa viwango vinavyostahili vya usanii ikiwa ni pamoja na kudhibiti maonyesho na usambazaji wa filamu za michezo ya kuigiza kiholela," alisema .

No comments:

Website counter