Monday, December 13, 2010

WATAKA KUMJUA 'DINHO', SOMA APO CHINI...

Jina lake halisi anaitwa RONALDO DE ASSIS MOREILA, ila sisi wadau pamoja na wabrazili wenyewe tumezoea kumuita RONALDINHO! Ni mmoja kati ya wanasoka hodari kupata kutokea Duniani na kipenzi cha wapenzi wengi wa soka Duniani. Amezaliwa March 21 - 1980 uko Porto Alegre nchini Brazil akiwa ni mtoto wapili kuzaliwa akitanguliwa na kaka yake mkubwa ambaye anaishi nae nyumba moja popote anapoenda kucheza soka pia ndio meneja wake anayemsimamia kilakitu aitwae 'ASSIS' ambaye kama una ishu yoyote ya kumuhitaji 'Dinho' basi lazma kwanza umuone uyu kaka m2 laa sivyo humpati Ng"ooooo tupilia mbali kumshika mkono! Ameshakuwa mwanasoka bora wa Dunia mara 2 mfululizo mwaka 2004 na 2005. Baba yake JOAO MOREIRA alikuwa ni Mfanyakzi wa Bandari uko Brazili ingawa alifariki kwa ugonjwa wa moyo wakati Dinho akiwa na umri wa miaka 8 na mama yake DONA MIGUELINA DE ASSIS ni muuguzi kitaaluma! Ni miongoni mwa wanasoka matajiri zaidi Duniani mwenye kufanya kazi na makampuni makubwa duniani kama vile Nike Pepsi, Danone, Cadbury Schweppes, Aspire na Levono. Ana majumba ya kutisha uko Barcelona, Milan na uko kwao Rio de jeneiro Brazil pamoja na kumiliki magari ya kifahari aina ya Marcedes benz cls na E- class, Ferari na mengineyo. Jamaa ana mtoto mmoja aitwae JOAO ambalo ni jina la marehemu babake na amezaa na mcheza shoo mmoja wa Club daah, kume huyu jamaa ni walewaleeee! kujua ufundi wake wa kuuchezea mpira, chec apo chini ujionee...

No comments:

Website counter