Thursday, December 30, 2010

MAMBO 6 USIYOYAJUA KUHUSU MSHAMBULIAJI MAROUANE CHAMAKH WA ARSENAL YA ENGLAND...


1. Anaitwa MAROUANE MOUSTAFA CHAMAKH aliyezaliwa Tar 10 Jan 1984 huko Tonneins karibu na mto Garonne nchini Ufaransa. 2. Baba yake Moustafa Chamakh aliingia Ufaransa mwaka 1979 kama mkimbizi akitokea kwao Casablaca nchini Morocco. 3. Alikuwa na akili sana darasani na haswa kwenye somo la Hesabu na mpaka sasa mbali na soka pia ana shahada ya Uhasibu inayomuwezesha kufanya kazi ya Uhasibu kwenye Kampuni yoyote ile ofisini. 4. Amemfungulia kaka yake ABDOU kampuni ya uwakala na kusafirisha magari sehemu mbalimbali Duniani na sikumoja moja akipata muda huwa anakwendaga ofisini kwa kaka yake na kumsaidia kufanya mahesabu ya kampuni ili kichwa chake kisidumae! 5. Chakula anachopenda huyu bwana ni Tambi za nyama pamoja na Viazi. Rafiki yake mkubwa ndani ya timu ya Arsenal ni kiungo TOMAS ROSICK ambaye huwa wanalala wote chumba kimoja Hotelini wanapokuwa ugenini sehemu yoyote inapocheza timu yake ya ARSENAL ya Uwingereza, upoo apoooo....

No comments:

Website counter