Wednesday, October 27, 2010

TUTAKUKUMBUKA PWEZA 'PAUL'...


Dunia nzima itamkumbuka Pweza huyu mwenye vituko aitwae 'PAUL' ambaye alikuwa bingwa wa utabiri Duniani baada ya kutabiri kwa usahihi mechi zoote ilizocheza timu ya Taifa ya Ujerumani kwenye kombe la Dunia lililofanyika nchini Afrika Kusini. Pweza PAUL aliyekuwa anaishi nchini Ujerumani, amefariki leo asubuhi akiwa na umri wa miaka 2 na miezi 9 na kwa kawaida Pweza huwa haishi zaidi ya miaka miwili, kwa maana hiyo Paul tayari alikuwa ni 'Mzee' saanaaa! Dunia itamkumbuka Paul kama PWEZA maarufu zaidi kuwahi kutokea Duniani...

No comments:

Website counter