Wednesday, October 13, 2010

BWANA KAIJAGE, NILIJUA YATAKUFIKA SIKUMOJA, NA SASA YAMETIMIA...


Kwako bwana mkubwa FLORIAN KAIJAGE! Wewe ni Mwandishi wa habari kama mimi ingawa wewe ni Mwandamizi, na kwenye kumbukumbu zangu ninakumbuka apo mwanzoni kabla hujakikwaa 'cheo' cha Usemaji wa Shirikisho la Soka la Tanzania 'TFF' ulikuwa ni mtu muungwana usiye na makuu, ila baada ya kupata cheo hicho cha usemaji apo TFF ndipo ulipoonyesha tabia yako halisi ya kutaka watu na haswa waandishi wa habari wakutukuze na kukuona Mungu m2! Ulishindwa kushughulikia matatizo ya waandishi wa habari na matokeo yake ulizidi kuwagandamiza wakati sie tulikuona kama mwenzetu, kwakweli kila m2 alikushangaa! Tatizo hukujua icho cheo kina mwisho wake na utarudi mtaani kama kawa, maana nakumbuka kusikia malalamiko ya wandishi wengi ambao wengi wao walikutakia 'MABAYA' kutokana na jinsi ulivyowatenda! Ivi unakumbuka 'kile kitu' nilichokuwa nakifatilia kwako ukawa unanisumbua bila sababu pamoja na mabosi wako kukwambia unipatie? Au hujui nasi tuko 'Busy' na tuna kazi zetu tena 'nyiingi' ila tunajaribu kuiba muda wetu kufatilia alafu eti unanizingua! Haya sasa umelitia aibu Taifa tena mbele ya Rais na matokeo yake icho kibarua alichoringia kimeota 'majani' kama sio 'kichaka', so tutakutana mtaani Kaka Kai....

3 comments:

Anonymous said...

Ben kumbuka usimtukane mamba kabla ya kuvuka mto na usiwatukane wakunga wakati uzazi ungalipo. inaonyesha ulikuwa na kinyongo sana na huyo Kaijage. lakini elewa kuwa Kaijage ametolewa kama mbuzi wa kafara tu, na wewe kama binadamu ilitakiwa kunyamaza kimya na kuliwacha swala hili lipite kama litakavyopita kwani muungwana akikosewa hamuombei mabaya aliyemkosea bali humuachia mungu. upande mwengine sisi sote ni binadamu na hakuna binadamu aliye mkamilifu na kumbuka sie sote tupo katika uwanja huu huu wa kutafuta maisha isije yaliomkuta fungo na kibwengo naye yakamkuta. huo mtazamo wangu.
mdau UK.

Issa said...

Hilo ndio tatizo hasa linalosumbua bala letu la afrika ,mtu akipewa cheo tu! hata wenzake ambao walikua wafanyakazi wenzake anawadhalau sana.Lakini hawa wenzetu wazungu wao hata urais akiwa ndani ya club au hotel flani au hata mtaani tu ni mtu wakawaida tu,,sio mtu wakujitia juuu kama Mungu,,kumbukeni msemo wa CHEO NI DHAMANA,,hivi wewe Kinya siku utapewa uwazili utaenderea kuchati na wadau hapa kwenye blog?Ha,ha

Anonymous said...

mmmh leo kasheshe! ben huyu mtu alikuudhi kias gan ww? wakat mwingine lakn ni vizur kumchana mtu laiv ili ajifunze...haina maana kunyamaza na kinyogo eti kwakuogopa watu watakuonaje? kwan yy alivofanya hakujua watu watamuonaje? tena tu mie naona ungempigia sim na kumwambia au cku ukikutana nae by chanc tel him liv bana haina maana kunyamaza nyamaza wakat yy alikuona ww kirago.

Website counter