Friday, October 22, 2010

BAADA YA KUPOKONYWA 'MADOLARY' YA BIG BROTHER, MUNYA AULA KWAO ZIMBABWE...


Mshiriki aliyeshika nafasi ya pili katika shindano la Big Brother Africa MUNYARADZI CHIDZONGA 'MUNYA' kutoka ZIMBAMBWE, amedondokewa na 'neema' nyingine na kuiaga rasmi 'NJAA' iliyokuwa ikimkabili baada wananchi mbalimbali wa nchi hiyo kumchangia Madolary zaidi 300,000 kwenye Account maalum iliyofunguliwa kwa ajili yake na Raisi wa nchi hiyo Mheshimiwa sana ROBERT MUGABE! Pamoja na Rais Mugabe kuchangia kutunisha Account hiyo pia juzi amemualika IKULU ya nchi hiyo kwenda kumpongeza kwa hatua aliyofikia kwenye Mtanange huo wa Big Brother, na MUNYA alimueleza wazi Rais MUGABE jinsi gani tangtu akiwa mdogo alivyokuwa na ndoto za kukutana nae Uso kwa Uso na hatimaye ndoto zake zikatimia juzi tena ndani ya jumba 'takatifu' la nchi hiyo aka 'IKULU', haaa haaaa ebu na sisi tufanye mpango wa kuchangia japo pesa kidogo mshiriki wetu mwisho ili nae akakiendeleze kituo chake kiduchu cha mafuta kule 'MANUNGU' Morogoro jamani na alafu Presidaaa nae amwite 'IKULU' kama alivyomuita HASHIMU THABEET sikuile etii eeeeh...

No comments:

Website counter