Wednesday, September 8, 2010

MPAKISTANI AKAMATWA KWA KUCHANA NOTI YA SH ELFU 5 HADHARANI...


POLISI mkoani Mwanza imemtia hatiani Raia mmoja wa Pakistani kwa tuhuma za kuchana NOTI ya sh elfu 5 HADHARANI. Tukio jili lilitokea jana majira ya saa 5 asubuhi katika uwanja wa ndege wa Mwanza wakati abiria huyo na wengineo wakisubiri kukagukiwa ili kuingia kwenye Ndege ya Precision tayari kwa safari ya kurudi Dar! Kamanda wa Polisi Mwanza Bw SIMON SORO alithibitisha kukamatwa kwa Mpakistani huyo baada ya kushuhudiwa akiichana Noti hiyo vipande vipande ndipo abiria wengine walioshikwa na hasira kwa kitendo icho cha Dharau na ukosefu wa adabu walipomuuliza sababu ya kuchana Noti hiyo lakini hakutoa majibu ya kuridhisha ndio walipowaita Polisi walio karibu na kumshughulikia pamoja na kukusanya vipande vyote vya pesa iyo kama ushahidi! Haa jamni iyo ni fedhea kubwa na yafaa apigwe Faini na Kifungo juu ili iwe fundisho kwa wengine wenye Dharau kama yeye maana kitendo icho nenda kakifanye nchi nyingine yoyote Hadharani uone utakavyofanywa!

2 comments:

Irene said...

Hana adabu kabisa anastahili faini na kifungu juu ili iwe fundisho kwa wengine pia.

Anonymous said...

he he he he he rudisha kwao huyo.hao ndo wale uhamiaji ilikua ikiwauzia uraia laki sita.kazi ipo

Website counter