Tuesday, June 15, 2010

MNAMJUA HUYU BWANA?....


Huyu pembeni yangu ni mshambuliaji hatari wa zamani wa kimataifa wa Tanzania ZAMOYONI MOGELLA aka 'Golden Boy'. Huyu bwana ni mfungaji mahiri wa zamani ambae hajawahi kutokea nchini ingawa kuna baadhi walijaribu kufikia kiwango chake! Alishawahi kuzichezea SIMBA na YANGA mpaka TAIFA STARZ kwa nyakati tofauti, ni mzaliwa wa MOROGORO ambako pia ndiko alikoanzia soka lake mpaka kuichezea TUMBAKU ya Morogoro ambako alionekana na kuchanua na na mimi binafsi ninamsifu kwa kuwa ni mmoja kati ya wachezaji wachache wa zamani nchini walioyapatia maisha kuliko wengine maarufu waliishia kwenye pombe na umasikini wa kutupwa na kwasasa najishughulisha na Biashara! Je wadau mnaomkumbuka huyu bwana na vitu alivyokuwa anavifanya uwanjani enzi hizo mna yapi ya kusema juu yake? Ebu Mwageni data zetu jamani...

4 comments:

Anonymous said...

huyu zamoyoni mogella sasa hivi anashughulika na nini?

Anonymous said...

Kwasasa Mogella ni mfanyabiashara jijini. BEN.

Anonymous said...

Yaani nilikuwa nafurahi sana kusikia jina lake wakati wa mpira, sasa mimi nilikuwa moshi kwa hivyo ilikuwa kupita kwenye radio tu, na unasikia - Zamoyoni Mogella, Zamoyoni Mogella....we acha bwana

Anonymous said...

Enzi hizo lazima usikie chama na mogella yani acha tu longtime sana Ben...

Website counter